Briggs & Stratton 2691184-00 Operator's Manual page 69

Hide thumbs Also See for 2691184-00:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Kaza kwa vidole, kisha kaza ukitumia spana kama
inavyoonyeshwa katika Kielelezo 12.
• 180 in-lbs (20 Nm), AU
• Mzunguko 1/2 wakati unaweka tena plagi asilia ya spaki.
Mzunguko 1/4 wakati unaweka plagi mpya ya spaki.
Sukuma Trekta kwa Mikono
Ili kusukuma trekta, fanya yafuatayo:
1. Zima swichi ya PTO (A, Kielelezo 13).
2. Zima injini.
3. Vuta sehemu ya gia ili ifunge ndani ya eneo lililo wazi.
4. Trekta inaweza kusukumwa kwa mikono
Onyo
Kukokota kifaa kutasababisha uharibifu kwenye klachi na gea.
Usitumie gari jingine kusukuma au kukokota mashine hii
Usisongeze wenzo wa kubadilisha gia wakati injini
imewashwa.
Vifaa Vinavyokokotwa
1. Kokota tu na mashine ambayo ina sehemu ya kuvuta
iliyoundwa ili kukokota.
2. Usiambatanishe vifaa vilivyovutwa ispokuwa katika sehemu
ya kuvutia.
3. Fuata mapendekezo ya mtengenezaji kuhusu kipimo cha
uzito wavifaa vilivyokokotwa na kuhusu kukokota kwenye
miteremko kama ilivyoorodheshwa.
• Jumla ya juu zaidi ya uzito (trela na mzigo) ni pauni
400.
• Upeo wa pauni 20 kwa futi juu au chini kwenye ulimi.
• Nenda kutoka kipimo cha digrii 10 kwenye mteremko
wowote.
4. Kamwe usiwaruhusu watoto au watu wengine kuingia ndani
au juu ya vifaa vinavyokokotwa.
5. Kwenye miteremko, uzito wa kifaa kinachovutwa unaweza
kusababisha kupoteza nguvu ya kukamata ardhi na
kupoteza udhibiti.
6. Nenda polepole na uwache nafasi ya ziada kwa ajili ya
kusimama.
7. Usihamishie kwenye gia huru na kuteremka kwenye
mteremko.
Hifadhi
Onyo
Usiwahi kuweka kifaa (kikiwa na mafuta) katika jengo
lililojifunga, na lbila hewa safi. Mivuke ya mafuta inaweza
kusafiri hadi kwenye chanzo cha mwako (kama vile tanuu,
hita ya kuchemshia maji, n.k) na kusababisha mlipuko.
• Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji,
au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto au vyanzo
vingine vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto
kwenye mvuke wa mafuta.
Kifaa
Zima PTO, weka breki ya kuegesha, na ondoa kiingiza stata.
Wacha mashine ipoe.
Maisha ya betri yatarefushwa ufunguo ukiondolewa. Weka betri
mahali baridi, pakavu na uiweke ikiwa na chaji wakati wa
kuhifadhi. Ikiwa betri imeachwa ndani ya kifaa, tengenisha kebo
ya hasi (negative).
Mfumo wa Mafuta
Mafuta yanaweza kuharibika yakihifadhiwa kwa zaidi ya siku
30. Mafuta yaliyoharibika yanasababisha mabaki ya asidi na
gundi kukusanyika katika mfumo wa mafuta au kwenye sehemu
muhimu za kabureta. Ili kuhifadhi usafi wa mafuta, tumia Briggs
& Stratton® Advanced Formula Fuel Treatment & Stabilizer,
inayopatikana mahali popote ambapo sehemu halisi za Briggs
& Stratton zinauzwa.
Hakuna haja ya kumwaga petroli kutoka kwenye injini ikiwa
kiimarishaji mafuta kimeongezwa kulingana na maagizo. Washa
injini kwa dakika 2 kuzungusha kisawashi katika mfumo wote
wa mafuta kabla ya kukiweka. Ikiwa petroli ilio kwenye injini
haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imiminwe kwenye
kontena iliyoidhinishwa. Endesha injini hadi isimame kutokana
na ukosefu wa fueli. Matumizi ya kiimarishaji mafuta kwenye
kontena ya uhifadhi yanapendekezwa ili kudumisha usafi.
Oili ya Injini
Wakati injini bado ina joto, badilisha oili yainjini.
Kabla ya kuwasha mashine baada ya kuwa kimehifadhiwa:
• Kagua viwango vyote vya mafuta na oili. Kagua vipengee
vyote vya udumishaji.
• Fanya kaguzi na taratibu zote zinazopendekezwa
zinazopatikana katika mwongozo huu.
• Wacha injini ipate joto kwa dakika kadhaa kabla ya kutumia.
69

Advertisement

Table of Contents
loading

Table of Contents