Briggs & Stratton 2691184-00 Operator's Manual page 63

Hide thumbs Also See for 2691184-00:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Hatari
Kuendesha kwenye miteremko, au karibu na maji, au maeneo
yaliyoshuka ghafla kunaweza kusababisha kupoteza udhibiti
na kubingirika.
• Kata nyasi kwenda juu na chini ya miteremko, sio kutoka
upande mmoja hadi mwingine.
• Punguza kasi na uwe makini zaidi kwenye miteremko.
• Usiendeshe kwenye miteremko ya zaidi ya digrii 10,
ambayo ni mwinuko wa futi 3.5 kwenye umbali wa futi 20.
• Kaa umbali wa sawia na ya mashine mbili za kukatia nyasi
na eneo lenye maji, kuta, au maeneo yaliyoshuka ghafla.
• Epuka kukata nyasi zilizo na majimaji au unyevunyevu.
• Usiendeshe mashine katika hali yoyote ambapo nguvu
ya magurudumu kukamata chini, uendeshaji au ustawi
hauaminiki. Magururdumu yanaweza kuteleza hata kama
magurudumu yamesimamishwa.
• Epuka kuanza au kusimama kwenye mteremko.
• Usifanye mabadiliko ya ghafla katika kasi au mwelekeo.
• Piga kona polepole na kwa utaratibu.
• Kuwa mwangalifu unapoendesha mashine nyenye vifaa
vya kukamata nyasi au viambatisho vingine. Vinaweza
kuathiri ustawi wa mashine hii.
• Fuata mapendekezo ya mtengenezaji kuhusu kipimo cha
uzito kwa vifaa vilivyokokotwa na ukokotaji kwenye
miteremko (rejelea Vifaa Vinavyokokotwa ).
5. Hakikisha eneo la kuendeshea halina watu waliosimama
kando, hasa watoto.
Hatari
Kifaa hiki cha kukatia nyasi kina uwezo wa kukata mikono na
miguu.
• Zima mashine ya kukatia nyasi wakati watoto au watu
wengine wapo karibu.
• Weka watoto mbali na eneo linalokatwa nyasi na chini ya
uangalizi mkubwa wa mtu mzima anayewajibika.
• Usiwahi kubeba watu, hasa watoto, hata kama visu
vimezimwa. Watoto wanaweza kuanguka na kujeruhiwa
vibaya sana au kuhitilafiana na uendeshaji salama wa
mashine. Watoto ambao wamewahi kubebwa na kifaa
hapo awali huenda wakatokea ghafla katika eneo
linalokatwa nyasi wakitaka kubebwa tena na wagongwe
au kusukumwa na mashine hiyo.
• Kuwa mwangalifu unapokaribia kona usizoweza kuona
mbali, vichaka, miti, au vitu vingine ambavyo vinaweza
kuzuia kuona.
Mita ya Saa
Mita ya saa inaonyesha saa jumla, saa za safari, na saa ya
kidijitali. (Kielelezo 3).
Onyesha Saa Jumla, Saa za Safari, na Saa
Kumbuka: Wakati unapowasha kifaa, Saa Jumla zinaonyeshwa.
Saa Jumla zitawekwa upya kiotomatiki hadi 0 baada ya kufikia
999.9.
1. Bonyeza MODI (MODE) kwa chini ya sekunde moja ili uone
Saa za Safari.
2. Bonyeza WEKA UPYA (RESET) kwa zaidi ya sekunde tatu
ili uweke upya Saa za Safari kuwa 0.
3. Bonyeza MODI (MODE) kwa chini ya sekunde moja ili uone
Saa. Bonyeza MODI (MODE) kwa zaidi ya sekunde tatu.
Saa zitaonekana kwenye skrini. Bonyeza WEKA UPYA
(RESET) ili kubadilisha saa. Bonyeza MODI (MODE) kwa
chini ya sekunde moja ili uhifadhi mpangilio. Dakika
zitaonekana kwenye skrini. Bonyeza WEKA UPYA (RESET)
ili kubadilisha dakika. Bonyeza MODI (MODE) kwa chini ya
sekunde moja ili uhifadhi mpangilio.
4. Bonyeza MODI (MODE) kwa chini ya sekunde moja ili urudi
kwenye Saa Jumla.
Majaribio ya Mfumo wa Usalama wa
Intaloki
Kifaa hiki kimewekwa Mfumo wa Usalama wa Intaloki. Usijaribu
kuhitilafiana na switchi/vifaa.
Onyo
Mashine ikikosa kupita jaribio la usalama, usiiendeshe.
Tembelea muuzaji aliyeidhinishwa.
Jaribio la 1 — Injini HAIPASWI kuwaka ikiwa:
• Swichi ya PTO IMEWASHWA, AU
• Pedali ya breki haijasukuwa kabisa (breki za kuegesha
ZIMEZIMWA).
Jaribio la 2 — Injini INAPASWA kuwaka na kuguruma ikiwa:
• Mwendeshaji amekalia kiti, NA
• Swichi ya PTO IMEWASHWA, AU
• Pedali ya breki imesukumwa kabisa (breki za kuegesha
ZIMEWASHWA).
Jaribio la 3 — Injini inafaa IZIME ikiwa:
• Mwendeshaji akiamkia kiti. .
Jaribio la 4 — Kagua Muda ambao Visu vya Kukatia Nyasi
Vinachukua Kusimama
Visu vya kukatia nyasi na mkanda wa kuendeshea mashine ya
kukatia nyasi zinafaa kusimama kabisa ndani ya sekunde tano
baada ya swichi ya PTO kuzimwa. Ikiwa mkanda wa mashine
ya kukatia nyasi hautasimama ndani ya sekunde tano,
mtembelee muuzaji aliyeidhinishwa.
Jaribio la 5 — Ukaguzi wa Chaguo la Ukataji Nyasi Ukirudi
Nyuma (RMO)
• Injini inafaa kuzima ikiwa utajaribu kurudi nyuma wakati
swichi ya PTO imewashwa na Chaguo la Ukataji Nyasi
Ukirudi Nyuma (RMO) halijawezeshwa.
63

Advertisement

Table of Contents
loading

Table of Contents