Briggs & Stratton 2691184-00 Operator's Manual page 64

Hide thumbs Also See for 2691184-00:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
• Taa ya Chaguo la Ukataji Nyasi Ukirudi Nyuma (RMO)
inafaa iwake wakati RMO imewezeshwa.
Hatari
Kukata nyasi ukirudi nyuma kunaweza kuwa hatari kwa
waliosimama kando. Ajali za kuhuzunisha zinaweza kutokea
ikiwa mwendeshaji hayuko makini kwa kuwepo kwa watoto.
Usiwahi wezesha Chaguo ya Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma
(RMO) ikiwa watoto wapo. Mara nyingi watoto huvutiwa na
mashine hiyo na shughuli ya ukataji nyasi.
Anzisha Trekta na Injini
Kagua na Uongeze Oili ya Injini
Tumia oili Zilizoidhinishwa na Hakikisho la Briggs & Stratton
ili kupata utendakazi bora. Oili nyingine za usafishaji
zinakubalika ikiwa zimebainishwa kwa huduma ya SF, SG,
SH, SJ au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum.
Hali joto ya nje inaamua mnato sahihi wa oili kwa injini. Tumia
chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya nje
inayotarajiwa.
A
SAE 30 *
B
10W-30 **
C
Synthetic 5W-30
D
5W-30
*Chini ya 40°F (4°C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa kuwasha
**Zaidi ya 80°F (27°C) matumizi ya 10W-30 huenda yakasababisha matumizi zaidi
ya oili. Kagua kiwango cha oili mara nyingi zaidi.
1. Weka trekta katika eneo tambarare (Kielelezo 4).
2. Zima injini na kisha uondoe ufunguo wa kuwasha.
3. Safisha eneo la kujazia oili kutokana na vifusi vyovyote.
4. Ondoa kifaa cha kupima oili na ukipanguse ukitumia
kitambaa safi.
5. Ingiza kabisa kifaa cha kupima oili.
6. Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili.
Inafaa iwe kwenye alama inayoonyesha IMEJAA (FULL)
kwenye kifaa cha kupima oili.
7. Ikiwa IMEJAA, ingiza kijiti cha kupima oili na ukaze vizuri.
64
8. Ikiwa CHINI (LOW), ongeza oili polepole ndani ya kopo la
oili ya injini (rejelea Mapendekezo ya Oili ). Usijaze kupita
kiasi. Baada ya kuongeza oili, subiri dakika moja, kisha
ukague kiwango cha oili.
Ongeza Mafuta
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
• Petroli safi, freshi, isiyo na lead (unleaded).
• Kiwango cha chini zaidi cha okteni 87 / 87 AKI (91 RON).
Kwa matumizi ya maeneo ya nyanda za juu, tazama hapa
chini.
• Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasohol) inakubalika.
Notisi Usitumie petroli ambayo haijaidhinishwa, kama vile
E15 na E85. Usichanganye oili kwenye petroli au kurekebisha
injini ili itumie mafuta mbadala. Utumizi wa mafuta ambayo
hayajaidhinishwa yatasababisha uharibifu wa vipengele vya
injini, jambo ambalo halijasimamiwa na hakikisho.
Ili kulinda mfumo wa mafuta kutokana na utengenezaji wa gundi,
changanya kiimarishaji mafuta ndani ya mafuta. Tazama Hifadhi.
Mafuta yote sio sawia. Iwapo matatizo ya kuwasha au
utendakazi yatatokea, badilisha unakonunua mafuta au
ubadilishe aina. Injini hii imeidhinishwa kuendeshwa kutumia
petroli. Mfumo wa kudhibiti mafukizo wa injini hii ni EM (Engine
Modifications (Marekebisho ya Injini)).
Mahitaji ya Maeneo Yaliyo Juu:
• Katika mwinuko zaidi ya fiti 5,000 (mita 1,524), kiwango
cha chini cha okteni 85//85 AKI (89 RON) cha petroli
kinakubalika.
• Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa
juu yanahitajika ili kudumisha uambatanaji na sera ya
mafukizo. Uendeshaji bila marekebisho haya unaweza
kusababisha kupunguka kwa utendakazi, matumizi ya
mafuta kuongezeka, na mafukizo kuongezeka. Wasiliana
na Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhibishwa
kwa maelezo ya marekebisho ya mwinuko wa juu.
• Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya futi 2,500
(mita 762) na marekebisho ya mwinuko wa juu
hayapendekezwi.
.
• Kwa injini za Uingizaji Mafuta wa Kielektroniki (EFI),
hakuna marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika.

Advertisement

Table of Contents
loading

Table of Contents