Briggs & Stratton 080000 Operator's Manual page 41

Hide thumbs Also See for 080000:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Ongeza Oili
Hakikisha injini inadumisha mizani.
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5). Futa oili kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili ukitumia kitambaa safi.
2.
Polepole weka oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo 5). Usijaze
kupita kiasi.  Subiri dakika moja, na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 5) kwenye kifaa cha kupima
kiwango cha oili.
5.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
6.
Unganisha waya wa plagi ya spaki kwenye plagi ya/za spaki. Tazama sehemu
ya Kuondoa Oili.
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa
ONYO 
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
NOTISI 
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza
kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako
na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Povu la Hewa
1.
Legeza au uondoe vifaa vya kufunga (A, Kielelezo 14), iwapo vipo.
2.
Fungua au uondoe kifuniko (B, Kielelezo 14).
3.
Kwa uangalifu ondoa elementi ya povu (C, Kielelezo 14) kutoka kwenye sehemu ya
chini ya chujio la hewa.
4.
Osha elementi ya povu (C, Kielelezo 14) kwenye sabuni oevu na maji. Finya
elementi ya povu ukitumia mikono yako ndani ya kitambaa kavu mpaka ikauke.
5.
Tumbukiza elementi ya povu (C, Kielelezo 14) ndani ya oili safi ya injini. Ili kuondoa
oili ya injini isiyohitajika kwenye elementi ya povu, ifinye ukitumia mikono yako
ndani ya kitambaa kavu.
6.
Sakinisha elementi ya povu (C, Kielelezo 14) kwenye sehemu ya chini ya chujio la
hewa.
7.
Funga au weka kifuniko (B, Kielelezo 14) na ufunge vizuri ukitumia bizimu.
Hakikisha kwamba umekaza vizuri.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 15).
2.
Ondoa chujio (C, Kielelezo 15).
3.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo 15), iwapo kipo, kwenye chujio (C).
4.
Ili kuondoa uchafu usiotakikana kwa utaratibu gongesha chujio kwenye eneo gumu.
Ikiwa chujio ni chafu libadilishe kwa chujio jipya.
5.
Osha kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo 15), iwapo kipo, kwenye sabuni oevu
na maji. Acha kisafishaji cha mwanzo kikauke kabisa. Usiongeze oili kwenye
kisafishaji cha mwanzo.
6.
Funga kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo 15) kilichokauka, ikiwa kipo, kwenye
chujio (C).
7.
Sakinisha chujio (C, Kielelezo 15).
8.
Sakinisha kifuniko (B, Kielelezo 15).
Hifadhi
Mfumo wa Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Kuhifadhi Mafuta
Kwa sababu taa za moto au vyanzo vingine vya mwako vinaweza kusababisha
milipuko, hifadhi mafuta au kifaa mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji,
au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto.
KUMBUKA: Miundo mingine ina tangi la mafuta la uhifadhi wima ambao unaruhusu
injini kuinama kwa ajili ya udumishaji au uhifadhi (C, Kielelezo 16). Usihifadhi ikiwa wima
wakati tangi la mafuta limejaa kupita kiwango cha alama ya kiwango cha mafuta (D),
iwapo ipo. Kwa maagizo zaidi, rejelea mwongozo wa kifaa.
Weka injini bila kuinama (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A,
Kielelezo 6) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kuzidi shingo ya tangi la
mafuta (B).
Mafuta yanaweza kuganda yanapohifadhiwa kwenye kontena ya uhifadhi kwa zaidi ya
siku 30. Inapendekezwa kutumia kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya ethanoli
kwenye kontena ya kuhifadhi mafuta. Hii inafanya mafuta kukaa yakiwa safi na
kupunguza matatizo yanayohusiana na mafuta au uchafu katika mfumo wa mafuta.
Unapojaza kontena hiyo ya mafuta kwa mafuta, ongeza kiimarishaji mafuta bila
alcoholi kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtenegenzaji. Ikiwa petroli ndani ya injini
haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imwagwe kwenye kontena iliyoidhinishwa.
Endesha injini hadi mafuta yaishe.
Oili ya Injini
Wakati injini bado ina joto, badilisha oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kubadilisha Oili
ya Injini.
Kutatua Matatizo
Usaidizi
Ili kupata usaidizi, wasiliana na muuzaji wa karibu au nenda
kwenyeBRIGGSandSTRATTON.COM au piga simu kwa nambari 1-800-444-7774
(nchini Marekani).
Maelezo na Sehemu za Udumishaji
Vipimo Maalum
Modeli: 080000
Unyonyaji Mafuta
7.63 ci (125 cc)
Shimo
2.362 in (60 mm)
Mpigo
1.75 in (44,45 mm)
Kiwango cha Oili
15 oz (,44 L)
Pengo la Plagi ya Spaki
.020 in (,51 mm)
Mkufu wa Plagi ya Spaki
180 lb-in (20 Nm)
Pengo la Hewa
.006 - .014 in
(,15 - ,36 mm)
Mwanya wa Vali ya
.004 - .008 in
Kuingiza Hewa
(,10 - ,20 mm)
Mwanya wa Vali ya
.004 - .008 in
Ekzosi
(,10 - ,20 mm)
Vipimo Maalum
Modeli: 093J00
Unyonyaji Mafuta
9.15 ci (150 cc)
Shimo
2.583 in (65,60 mm)
Mpigo
1.75 in (44,45 mm)
Kiwango cha Oili
15 oz (,44 L)
Pengo la Plagi ya Spaki
.020 in (,51 mm)
Mkufu wa Plagi ya Spaki
180 lb-in (20 Nm)
Pengo la Hewa
.006 - .014 in
(,15 - ,36 mm)
Mwanya wa Vali ya
.004 - .008 in
Kuingiza Hewa
(,10 - ,20 mm)
Mwanya wa Vali ya
.004 - .008 in
Ekzosi
(,10 - ,20 mm)
Modeli: 090000
8.64 ci (140 cc)
2.495 in (63,4 mm)
1.75 in (44,45 mm)
15 oz (,44 L)
.020 in (,51 mm)
180 lb-in (20 Nm)
.006 - .014 in
(,15 - ,36 mm)
.004 - .008 in
(,10 - ,20 mm)
.004 - .008 in
(,10 - ,20 mm)
Modeli: 100000
9.93 ci (163 cc)
2.688 in (68,28 mm)
1.75 in (44,45 mm)
15 oz (,44 L)
.030 in (,76 mm)
180 lb-in (20 Nm)
.006 - .014 in
(,15 - ,36 mm)
.004 - .008 in
(,10 - ,20 mm)
.004 - .008 in
(,10 - ,20 mm)
41

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

090000093j001000000

Table of Contents