Briggs & Stratton 080000 Operator's Manual page 39

Hide thumbs Also See for 080000:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Washa Injini
ONYO 
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu. Ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na mbali
na madirisha, milango na matundu.
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapowasha injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji
hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la
IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi
kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
ONYO 
Sehemu zinazozunguka zinaweza kunasa mikono, miguu, nywele, nguo, au
vifuasi na kupelekea kukatwa viungo au ngozi vibaya.
Endesha kifaa vilinzi vikiwa vimesakinishwa vizuri.
Weka mikono na miguu mbali na sehemu zinazozunguka.
Vua vipuli na uhakikishe kwamba nywele ndefu ziko mbali na sehemu
zinazozunguka.
Usivae nguo zilizolegea au vipengee vinavyoweza kushikwa.
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo kuteguka.
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
Aina za Mfumo wa Kuwasha
Kabla ya kuwasha injini, ni lazima ujue aina ya mfumo wa kuwasha ambao uko kwenye
injini yako. Injini yako ina mojawapo ya aina zifuatazo za mifumo ya kuwasha:
®
ReadyStart
na Mfumo wa Kuwasha kwa Hatua-1: Mfumo wa kuwasha wa
aina hii una choki otomatiki inayodhibitiwa na halijoto. Haina prima.
Mfumo wa Choki: Mfumo wa aina hii una choki ya kutumiwa katika mazingira
yenye baridi. Baadhi ya miundo ina kidhibiti cha choki tofauti huku miundo
mingine ina muunganiko wa choki na kidhibiti injini. Haina prima.
Mfumo wa Prima: Mfumo huu wa kuwasha una prima nayotumiwa kuwasha
katika mazingira yenye baridi. Haina choki kikuli.
KUMBUKA: Kifaa chako kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Rejelea mwongozo wa
kifaa ili utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia.
®
Choki, ReadyStart
na Mfumo wa Kuwasha kwa Hatua-1
1.
Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
2.
Zima vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo.
3.
Sogeza vali ya kufunga mafuta (A, Kielelezo 7), iwapo kipo, hadi eneo
linaloonyesha FUNGUA
4.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 7), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
5.
Sogeza kidhibiti cha choki (F, Kielelezo 8), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
6.
Sukuma swichi ya kuzima (D, Kielelezo 8), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha WASHA.
7.
Shikilia wenzo wa kuzima injini, iwapo upo, dhidi ya kishikio.
8.
Kwa uthabiti shikilia kishikio cha kamba ya kianzishaji (G, Kielelezo 7), iwapo kipo.
Vuta kishikio cha kamba ya kianzishaji (G) polepole hadi uhisi ugumu, kisha vuta
kwa haraka.
9.
Injini inapochemka, sogeza kidhibiti choki (F, Kilelelezo 8) hadi eneo linaloonyesha
FUNGUA.
KUMBUKA: Injini ikikosa kuwasha, nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au
upige simu kwa nambari 1-800-444-7774 (nchini Marekani).
Mfumo wa Prima
Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
1.
2.
Hakikisha kwamba umezima vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo.
3.
Sukuma swichi ya kuzima (A, Kielelezo 9), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha WASHA.
4.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 9), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
5.
Sukuma kitufe cha prima nyekundu (F, Kielelezo 9), mara tatu.
KUMBUKA: Prima haihitajiki wakati wa kuwasha upya injini iliyochemka.
KUMBUKA: Ukibonyeza kitufe cha prima mara nyingi sana, injini itafurika na itakuwa
gumu kuiwasha.
6.
Shikilia wenzo wa kuzima injini, iwapo upo, dhidi ya kishikio.
7.
Kwa uthabiti shikilia kishikio cha kamba ya kianzishaji (D, Kielelezo 9), iwapo kipo.
Vuta kishikio cha kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi ugumu, kisha vuta kwa
haraka.
Zima Injini
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Usikabe kabureta (iwapo ipo) ili kusimamisha injini.
1.
Achilia wenzo wa kuzima injini, iwapo upo.
2.
Sukuma swichi ya kuzima (D, Kielelezo 8), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha ZIMA.
3.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 7), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
SIMAMA.
4.
Baada ya injini kuzima, sogeza vali ya kufunga mafuta (A, Kielelezo 7), iwapo ipo,
hadi eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
Udumishaji
Maelezo ya Udumishaji
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi la
mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi ya spaki
uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au
mlipuko. Ikiwa injini imeinama katika mkao tofauti, haitaguruma kwa urahisi kwa sababu
ya kuchafuka kwa chujio la hewa au plagi ya spaki kwa oili au mafuta.
39

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

090000093j001000000

Table of Contents