Snapper SPX-100 Operator's Manual page 103

Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Soma kanuni hizi za usalama na zifuate kwa karibu. Kushindwa kutii kanuni hizi kunaweza kusababisha kupoteza
udhibiti wa kifaa, jeraha baya sana au kifo kwako, au kwa watazamaji, au hasara katika mali au kifaa. Deki hii
ya mashine ya kukatia nyasi ina uwezo wa kukata mikono na miguu na kurusha vitu. Ala ya pembe tatu
katika maandishi inamaanisha tahadhari muhimu au maonyo ambayo lazima yafuatwe.
UENDESHAJI WA KAWAIDA
1 Soma, elewa, na fuata maelekezo yote katika mwongozo
na katika kifaa kabla ya kuanza.
2 Usiweka mikono au miguu karibu na sehemu
zinazozunguka au chini ya mashine. Weka wazi kutokana
na ufunguaji wa uondoaji wakati wote.
3 Ruhusu tu watu wazima wanaowajibika, ambao
wanatambua maelekezo, kuendesha kifaa hicho (sheria za
ndani zinaweza kuzuia umri wa mwendeshaji).
4 Safisha eneo kutokana na vifaa kama vile mawe,
wanasesere, waya, n.k., ambavyo vinaweza kuokotwa na
kurushwa na ubapa wa kifaa.
5 Hakikisha eneo hilo halina watu wengine kabla ya kukata
nyasi. Simamisha kifaa ikiwa mtu yeyote ataingia eneo hilo.
6 Kamwe usipakie abiria.
7 Usikate nyasi kwa kurudi nyuma ispokuwa ikiwa inahitajika.
Daima tazama chini na nyuma kabla na wakati wa kuhama
kurudi nyuma.
8 Usielekeze nyezo yoyote ya ung'oaji kwa mtu yeyote.
Epusha kuacha nyezo ya ung'oaji ukutani au kizuizini.
Nyezo inaweza kurudi nyuma kumwelekea mwendeshaji.
Simamisha mabapa wakati wa kuvuka sehemu za
changarawe.
9 Usiendeshe mashine bila ya kikamata majani kizima,
ondoa kinga (kivuta upande), au vifaa vingine vya usalama
katika sehemu.
10 Punguza mwendo kabla ya kugeuka.
11 Kamwe usiwache kifaa kinachoenda bila ya
kushughulikiwa. Daima toa PTO, weka breki ya kuegesha,
simamisha injini, na ondoa kiingiza stata kabla ya kushuka.
12 Toa mabapa (PTO) wakati hukati nyasi. Zima injini na
subiri sehemu zote ziwe katika kusimama kwa kukamilika
kabla ya kusafisha mashine, kuondoa kikamata majani, au
kuondoa kizuia utendaji.
13 Endesha mashine tu wakati wa mchana au katika taa ya
mwangaza mzuri.
14 Usiendeshe kifaa hicho wakati wa athari ya kilevi au
madawa.
USAFIRISHA NA UHIFADHI
1 Wakati wa kusafirisha kifaa hicho kwenye trela la wazi,
hakikisha kinaelekea mbele, katika mwelekeo wa safari.
Ikiwa kifaa hicho kinaelekea nyuma, unyanyuaji wa upepo
unaweza kuharibu kifaa hicho.
2 Daima chunguza ujazaji upya wa mafuta salama na
utendaji wa mafuta wakati wa kujaza upya mafuta kifaa
baada ya usafirishaji au hifadhi.
3 Kamwe usiweke kifaa hicho (na mafuta) katika jengo
la wazi lenye upepo dhaifu. Mivuke ya mafuta inaweza
kusafiri hadi kwenye chanzo cha mwako (kama vile tanuu,
hita ya maji, n.k) na kusababisha mlipuko. Mvuke wa
mafuta pia ni sumu kwa binadamu na wanyama.
15 Chunga magari unaopendesha karibu na makutano ya
barabara.
16 Tumia uangalifu zaidi wakati wa kupakia au kushusha kifaa
hicho kwenye trela au gari kubwa.
17 Daima vaa kitu cha kulinda macho wakati wa kuendehsa
kifaa hiki.
18 Data inaonyesha kwamba waendeshaji, miaka 60 na zaidi,
wanahusika kwa asilimia kubwa majeraha yatokanayo na
nguvu ya nishati ya kifaa. Waendeshaji hawa wanapaswa
kutathmini uwezo wao ili kuendesha kifaa hicho kwa
usalama wa kutosha ili kujilinda wao wenyewe na wengine
kutokana na kujeruhiwa.
19 Fuata mapendekezo ya kiwandani kwa ajili ya uzito wa
matairi au uzito.
20 Kumbuka kwamba mwendeshaji anawajibika na ajali
zinazotokea kwa watu wengine au mali.
21 Madereva wote wanapaswa kutafuta na kupata maelekezo
ya kitaalam na mazoezi.
22 Daima vaa viatu vikubwa miguuni na suruali. Kamwe
usiendeshe ukiwa upo pekupeku au umevaa malapa.
23 Kabla ya kutumia, daima kwa kutazama kagua kwamba
mabapa na zana ya mabapa vipo, madhubuti, na salama.
Badilisha sehemu zilizochakaa au kuharibika.
24 Ondoa viambatanishi kabla ya: kujaza upya mafuta,
kuondoa kiambatanishi, kufanya marekebisho (ispokuwa
ikiwa marekebisho hayo yanaweza kufanywa katika
sehemu ya mwendeshaji).
25 Wakati mashine imeegeshwa, kuhifadhiwa, au imeachwa
bila ya shughulikiwa, punguza njia za kukata ispokuwa
ikiwa kufuli nzuri ya mekaniki inatumika.
26 Kabla ya kuonfoa mkao wa mwendeshaji kwa sababu
yoyote ile, weka breki ya kuegesha, toa PTO, zima injini, na
uonde kifunguo.
27 Kwa kupunguza hatari ya moto, weka kifaa hicho bila ya
nyasi, majani, na mafuta ya ziada. Usisimame au kufunga
breki kwenye majani makavu, nyasi, au vitu vinavyoungua.
4 Daima fuata maelekezo ya mwongozo wa injini kwa
maandalizi ya kuhifadhi kabla ya kuhifadhi kifaa hicho kwa
ajili ya vipindi vifupi na virefu.
5 Daima fuata maelekezo ya mwongozo kwa ajili ya hatua
nzuri za kuwasha kifaa wakati wa kukirejesha kifaa hicho
kwenye huduma.
6 Kamwe usiweke kifaa au kontena ya mafuta ndani ambapo
kuna mwako wa moto wa wazi au taa ya kibatali au stova,
kama vile hita ya kuchemshia maji. Kiache kifaa kipowe
kabla ya kukihifadhi.
sw
3

Hide quick links:

Advertisement

Table of Contents
loading

Table of Contents