Briggs & Stratton 080000 Operator's Manual page 56

Hide thumbs Also See for 080000:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Kufanyia Huduma Plagi ya Spaki
Kagua pengo la plagi ya spaki (A, Kielelezo  12) ukitumia pamba ya waya (B). Ikiwa
inahitajika, rekebisha pengo la plagi ya spaki.  Sakinisha na ukaze plagi ya spaki kwa
kiwango sahihi. Ili kupata maelezo maalum ya pengo na kukaza, rejelea sehemu ya
Maelezo.
KUMBUKA: Katika baadhi ya maeneo, kulingana na sheria za eneo husika ni
lazima kutumia plagi ya spaki ya kifaa kisichopitisha nishati ili kupunguza ishara
za kugurumisha. Ikiwa plagi ya spaki ya kifaa kisichopitisha nishati iliwekwa na
mtenegenezaji wa kifaa hicho, tu,ia aina sawa unapobadilisha.
Badilisha Oili ya Injini
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la
mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto
au mlipuko.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa njia sahihi. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma
au muuzaji ili kupata zana salama za kutupa au kutumia tena.
Kwa miundo ya Just Check & Add
kubadilisha oili, basi fuata utaratibu ufuatao.
Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa imezimwa lakini ina joto, tenganisha waya wa plagi ya spaki (D,
Kielelezo 13) na uiweke mbali na plagi ya/za spaki (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 14).
3.
Wakati unamwaga oili kutoka kwenye mrija wa kujazia oili wa upande wa juu (C,
Kielelezo 15), weka upande wa injini ulio na plagi ya spaki (E) ukiwa umeangalia
juu. Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
ONYO 
Unapomwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la mafuta
liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kupelekea moto au mlipuko.
Endesha injini hadi isimame kwa kukosa mafuta.
Ongeza Oili
Hakikisha injini inadumisha mizani.
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5). Futa oili kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili ukitumia kitambaa safi.
2.
Polepole weka oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo 5). Usijaze
kupita kiasi.  Subiri dakika moja, na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 5) kwenye kifaa cha kupima
kiwango cha oili.
5.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
6.
Unganisha waya wa plagi ya spaki kwenye plagi ya/za spaki. Tazama sehemu
ya Kuondoa Oili.
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa
ONYO 
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
NOTISI 
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza
kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
56
, hauhitaji kubadilisha oili. Ikiwa unahitaji
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako
na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Povu la Hewa
1.
Legeza au uondoe vifaa vya kufunga (A, Kielelezo 16), iwapo vipo.
2.
Fungua au uondoe kifuniko (B, Kielelezo 16).
3.
Kwa uangalifu ondoa elementi ya povu (C, Kielelezo 16) kutoka kwenye sehemu ya
chini ya chujio la hewa.
4.
Osha elementi ya povu (C, Kielelezo 16) kwenye sabuni oevu na maji. Finya
elementi ya povu ukitumia mikono yako ndani ya kitambaa kavu ili ikauke.
5.
Tumbukiza elementi ya povu (C, Kielelezo 16) ndani ya oili safi ya injini. Ili kuondoa
oili ya injini isiyohitajika kwenye elementi ya povu, ifinye ukitumia mikono yako
ndani ya kitambaa kavu.
6.
Sakinisha elementi ya povu (C, Kielelezo 16) kwenye sehemu ya chini ya chujio la
hewa.
7.
Funga au weka kifuniko (B, Kielelezo 16) na ufunge vizuri ukitumia
bizimu. Hakikisha kwamba umekaza vizuri.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 17).
2.
Ondoa chujio (C, Kielelezo 17).
3.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo 17), iwapo kipo, kwenye chujio (C).
4.
Ili kuondoa uchafu usiotakikana kwa utaratibu gongesha chujio kwenye eneo gumu.
Ikiwa chujio ni chafu libadilishe kwa chujio jipya.
5.
Osha kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo 17), iwapo kipo, kwenye sabuni oevu
na maji. Acha kisafishaji cha mwanzo kikauke kabisa. Usiongeze oili kwenye
kisafishaji cha mwanzo.
6.
Funga kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo 17) kilichokauka, ikiwa kipo, kwenye
chujio (C).
7.
Sakinisha chujio (C, Kielelezo 17).
8.
Sakinisha kifuniko (B, Kielelezo 17).
Kufanyia Huduma Mfumo wa Kupoesha
ONYO 
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Uchafu unaoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi na brashi, vinaweza
kushika moto.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
NOTISI 
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa mafuta. Tumia brashi
au kitambaa kavu kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa kwa kutumia hewa. Uchafu au vifusi vinaweza kuzuia
mtiririko wa hewa na kusababisha injini kuwa moto sana na hii kupelekea utendakazi
usioridhisha na injini kuwa na maisha mafupi.
1.
Tumia brashi au kitambaa kavu kuondoa vifusi kwenye grili ya kuingiza hewa.
2.
Weka viunganishaji, springi na vidhibiti vikiwa safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, bila uchafu wowote unaoweza
kuwaka moto.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha oili, ikiwa yapo, yakiwa safi.
Baada ya kipindi cha muda, mapezi ya kupoesha silinda yanaweza kukusanya vifusi
na kusababisha injini kuwa moto kupita kiasi. Uchafu huu hauwezi kuondolewa
bila kutenganisha sehemu kadhaa za injini. Ruhusu Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa
wa Briggs & Stratton kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa kama
ilivyopendekezwa kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Mfumo wa Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Kuhifadhi Mafuta
Kwa sababu taa za moto au vyanzo vingine vya mwako vinaweza kusababisha
milipuko, hifadhi mafuta au kifaa mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji,
au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto.
BRIGGSandSTRATTON.COM

Hide quick links:

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

090000093j001000000

Table of Contents