Briggs & Stratton 080000 Operator's Manual page 54

Hide thumbs Also See for 080000:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Washa Injini.
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo kuteguka.
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapowasha injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji
hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la
IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi
kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
ONYO 
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu. Ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na mbali
na madirisha, milango na matundu.
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
Aina za Mfumo wa Kuwasha
Kabla ya kuwasha injini, ni lazima ujue aina ya mfumo wa kuwasha ambao uko kwenye
injini yako. Injini yako itakuwa na mojawapo ya aina zifuatazo za mifumo ya kuwasha:
®
ReadyStart
na Mfumo wa Kuwasha kwa Hatua-1: Mfumo wa kuwasha wa
aina hii una choki otomatiki inayodhibitiwa na halijoto. Haina prima.
Mfumo wa Choki: Mfumo wa aina hii una choki ya kutumiwa katika halijoto
baridi. Baadhi ya miundo itakuwa na kidhibiti cha choki tofauti huku miundo
mingine itakuwa na muunganiko wa choki na kidhibiti injini. Haina prima.
Mfumo wa Prima: Mfumo huu wa kuwasha una prima nyekundu inayotumiwa
kuwasha katika hali joto baridi. Haina choki kikuli.
KUMBUKA: Kifaa chako kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Rejelea mwongozo wa
kifaa ili utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia.
®
ReadyStart
na Mfumo wa Kuwasha kwa Hatua-1
1.
Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
2.
Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Sogeza kizima mafuta (A, Kielelezo 7), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
FUNGUA
54
4.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 7), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
5.
Sukuma swichi ya kuzima (D, Kielelezo 8), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha WASHA.
6.
Shikilia wenzo wa kuzima injini (C, Kielelezo 9), iwapo upo, dhidi ya kishikio.
7.
Kwa uthabiti shikilia kishikio cha kamba ya kianzishaji (G, Kielelezo 7), iwapo kipo.
Vuta kamba ya kianzishaji (G) polepole hadi uhisi upinzani, na kisha, vuta kishikio
cha kamba ya kianzishaji kwa haraka.
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta
mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Inaweza kupelekea
mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka
wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na
kisha uvute haraka.
8.
Geuza swichi ya kianzishaji cha umeme, iwapo ipo, hadi eneo linaloonyesha
WASHA / ANZA.
NOTISI 
Ili kurefusha maisha ya kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo wa
sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko ya kuanzisha.
KUMBUKA: Injini ikikosa kuwasha, wasiliana na muuzaji wako wa ndani au nenda
kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au upige simu kwa nambari 1-800-444-7774
(nchini Marekani).
Mfumo wa Choki
1.
Kagua oili ya injini. Tazama sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
2.
Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Sogeza vali ya kufunga mafuta (A, Kielelezo 7), iwapo ipo, hadi eneo linaloonyesha
FUNGUA.
4.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 7), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
5.
Sogeza kidhibiti choki (F, Kielelezo 10) hadi eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
KUMBUKA: Kwa kawaida choki haihitajiki wakati wa kuwasha upya injini iliyochemka.
6.
Sukuma swichi ya kuzima (D, Kielelezo 10), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha WASHA.
7.
Shikilia wenzo wa kuzima injini (C, Kielelezo 9), iwapo upo, dhidi ya kishikio.
8.
Kwa uthabiti shikilia kishikio cha kamba ya kianzishaji (G, Kielelezo 7), iwapo kipo.
Vuta kishikio cha kamba ya kianzishaji (G) polepole hadi uhisi upinzani, kisha vuta
kwa haraka.
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta
mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Inaweza kupelekea
mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka
wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na
kisha uvute haraka.
9.
Geuza swichi ya kianzishaji cha umeme, iwapo ipo, hadi eneo linaloonyesha
WASHA/ANZA.
NOTISI Ili kurefusha maisha ya kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo
wa sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko ya kuanzisha.
10. Injini inapochemka, sogeza kidhibiti cha choki (F, Kilelelezo 10) hadi eneo
linaloonyesha FUNGUA.
KUMBUKA: Injini ikikosa kuwasha, wasiliana na muuzaji wako wa ndani au nenda
kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au upige simu kwa nambari 1-800-444-7774
(nchini Marekani).
Mfumo wa Prima
1.
Kagua oili ya injini. Tazama sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili
2.
Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Sukuma swichi ya kuzima (A, Kielelezo 11), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha WASHA.
4.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 11), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
5.
Sukuma kitufe cha prima nyekundu (F, Kielelezo 11), mara tatu (3).
KUMBUKA: Kwa kawaida prima haihitajiki wakati wa kuwasha upya injini iliyochemka.
BRIGGSandSTRATTON.COM

Hide quick links:

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

090000093j001000000

Table of Contents