Briggs & Stratton 090000 Operator's Manual page 10

Hide thumbs Also See for 090000:
Table of Contents

Advertisement

Available languages

Available languages

Ujumbe wa Usalama
ONYO
Bidhaa hii inaweza kukuweka hatarini mwa kemikali ikiwemo moshi wa injini ya petroli,
ambao unafahamika kusababisha saratani katika Jimbo la California, na kaboni
monoksidi, ambayo inafahamika kusababisha kasoro za kuzaliwa au madhara ya uzazi
katika Jimbo la California. Ili kupata maelezo zaidi nenda kwenye www.P65Warnings.
ca.gov.
ONYO
Injini za Briggs & Stratton
hazijaundwa kuzalisha nguvu za umeme au
®
kuendesha: vijigari vya kufurahia; vijigari vya kuendesha; vya watoto, burudani,
au magari ya barabara ya aina yote (ATVs); pikipiki; gari la kuendeshea juu ya
maji;bidhaa za ndege; au magari yaliyotumiwa katika matukio ya mashindano
yasiyowekewa vikwazo na Briggs & Stratton. Kwa maelezo kuhusu bidhaa za
mashindano ya uendeshaji magari, tazama www.briggsracing.com. Kwa matumizi
pamoja na vifaa na ATV za upande kwa upande, tafadhali wasiliana na Kituo
cha Matumizi ya Injini cha Briggs & Stratton, 1-866-927-3349. Matumizi ya injini
isivyofaa inaweza kusababisha majeraha mabaya au kifo.
ILANI: Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji
vifaa huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara
ya kwanza, hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama
ilivyobainishwa na maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini
itaharibika na haiwezi kukarabatiwa chini ya waranti.
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapoongeza mafuta
Zima injini. Kabla ya kufunua kifuniko, subiri angalau dakika mbili (2) ili
kuhakikisha injini imepoa.
Jaza tangi la mafuta ukiwa nje au katika eneo lenye hewa nyingi safi.
Usiweke mafuta mengi kupita kiasi kwenye tangi. Kwa ajili ya uvukizi wa
mafuta, usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo
vingine vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
Unapowasha injini
• Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji
hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
• Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
• Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la
IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi
kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
• Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
• Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
Unapofanyia huduma ya udumishaji
• Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la mafuta
liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
• Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi
la mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa
plagi ya spaki uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja
na kusababisha moto au mlipuko.
• Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo
sawa kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa
au kusababisha majeraha.
Wakati wa kuhifadhi mafuta au kifaa kikiwa na mafuta kwenye tangi la mafuta
• Kwa sababu taa za moto au vyanzo vingine vya mwako vinaweza kusababisha
milipuko, hifadhi mafuta au kifaa mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia
maji, au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto.
ONYO
Mwako wa injini usiokusudiwa unaweza kusababisha mshutuko wa umeme
au moto na kupelekea kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au
majeraha mabaya ya ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
• Tenganisha waya wa plagi ya spaki na uuweke mbali na plagi ya spaki.
• Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishaji cha
umeme.)
• Tumia zana sahihi pekee.
Unapokagua uwepo wa cheche:
• Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
• Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
10
ONYO
Sehemu zinazozunguka zinaweza kunasa mikono, miguu, nywele, nguo, au
vifuasi na kupelekea kukatwa viungo au ngozi vibaya.
• Endesha kifaa vilinzi vikiwa vimesakinishwa vizuri.
• Weka mikono na miguu mbali na sehemu zinazozunguka.
• Vua vipuli na uhakikishe kwamba nywele ndefu ziko mbali na sehemu
zinazozunguka.
• Usivae nguo zilizolegea au vipengee vinavyoweza kushikwa.
ONYO
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Vitu vinavyoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi, vinaweza
kushika moto.
• Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
• Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442,
kutumia au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa
na brashi, au lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama
ilivyobainishwa katika sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya
kufanya kazi. Mamlaka nyingine za majimbo au serikali ya kitaifa huenda zikawa na
sheria sawia; Rejelea Kanuni za Serikali ya KItaifa ya 36 CFR Sehemu ya 261.52.
Wasiliana na mtengenezaji asilia wa kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata
kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini
hii.
ONYO
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Ukinusa gesi
• Usiwashe injini.
• Usiwashe swichi za kiumeme.
• Usitumie simu katika eneo hilo.
• Ondoka kwenye eneo hilo.
• Wasiliana na idara ya wazima moto.
Unapoendesha kifaa
• Usiinamishe injini au kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
• Usikabe kabureta (iwapo ipo) ili kusimamisha injini.
• Usiwashe au kuendesha injini kamwe wakati kisafishaji hewa (iwapo kipo) au
chujio la hewa (iwapo lipo) vimeondolewa.
Unapohamisha kifaa hadi eneo nyingine
• Hakikisha tangi la mafuta ni TUPU au vali ya kufungia ipo katika eneo la kuonyesha
IMEFUNGWA.
ONYO
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda
ukawa umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
• Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu. Ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na mbali
na madirisha, milango na matundu.
• Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
• USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
• KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
ONYO
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa
haraka) kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko
unavyoweza kuachilia. Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika,
michubuko amu maungo kuteguka.
• Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
• kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
• Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

093j00080000100000

Table of Contents