Briggs & Stratton VANGUARD 10V000 Operator's Manual page 49

Hide thumbs Also See for VANGUARD 10V000:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Ili kulinda mfumo wa mafuta kutokana na utengenezaji wa gundi, changanya kiimarishaji
mafuta ndani ya mafuta. Tazama  Uhifadhi.  Mafuta yote sio sawia. Iwapo matatizo
ya kuwasha au utendakazi yatatokea, badilisha unakonunua mafuta au ubadilishe
aina. Injini hii imeidhinishwa kuendeshwa kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti mafukizo
wa injini za kabureta ni EM (Engine Modifications (Marekebisho ya Injini)). Mifumo ya
kudhibiti mafukizo kwa injini zilizo na unyonyaji mafuta kielektroniki ni ECM (Engine
Control Module (Moduli ya Kidhibiti Injini)), MPI (Multi Port Injection (Unyonyaji kwa
Matundu Kadhaa)) na ikiwa ina O2S (Oxygen Sensor (Sensa ya Oksijeni)).
Mwinuko wa Juu
Katika mwinuko wa zaidi ya futi 5,000 (mita1524), kiwango cha chini cha okteni 85 /85
AKI (89 RON) petroli inakubaliwa.
Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika ili kudumisha
utendakazi. Oparesheni bila marekebisho unaweza kusababisha kupunguka kwa
utendakazi, matumizi ya fueli yalioongezeka, na uchafuzi ulioongezeka. Wasiliana na
Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhibishwa kwa maelezo ya marekebisho ya
mwinuko wa juu. Oparesheni wa injini katika mwinuko wa chini ya futi 2,500 (mita 762)
na marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uinjizaji wa Fueli wa Kielektriki (EFI), hakuna marekebisho ya mwinuko wa
juu yanahitajika.
Ongeza Mafuta
Tazama Kelelezo: 15
Onyo
Fueli na mvuke wako unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Wakati wa kuongeza fueli
• Zima injini na uruhusu injini kupoa angalau dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko cha
fueli.
• Jaza tangi la fueli nje au katika eneo linaruhusu hewa kuingia vizuri.
• Usijaze tangi la fueli kupita kiasi. Ili kuruhusu upanukaji wa fueli, usijaze kupita
chini ya shingo la tangi la fueli.
• Hifadhi fueli mbali na cheche, miale iliyo wazi, taa za mwongozo, joto na vyanzo
vingine vya uwakaji.
• Angalia tundu, tangi, kifuniko na kurekebisha mara kwa mara kwa nyufa na uvujaji.
Badilisha ikiwezekana.
• Iwapo fueli itamwagika, subiri hadi ivukize kabla ya kuwasha injini.
1.
Safisha kifuniko cha fueli kutokana na uchafu. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la fueli kwa fueli (A, Kielelezo 15). Ili kuruhusu upanuzi wa fueli, usijaze
juu ya chini ya shingo la tangi la fueli (B).
3.
Sakinisha upya kifuniko cha fueli.
Washa na Uzime Injini
Tazama Kielelezo: 16 
Washa Injini
Onyo
Uvutaji nyuma kwa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa
haraka) kutavuta mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza
kuachilia. 
Inaweza kupelekea mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. 
• Wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi inakuwa
gumu kuvuta na kisha uvute kwa haraka ili kuzuia kuvutwa nyuma kwa haraka. 
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana. 
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo. 
 Wakati wa Kuwasha Injini 
• Hakikisha kwamba plagi ya spaki,mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji hewa
(iwapo kipo) vimefungwa na kukazwa. 
• Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa. 
• Injini ikifurika, weka choki (ikiwa ipo) katika eneo la kuonyesha FUNGUA au
ENDESHA, songeza kidhibiti injini (ikiwa kipo) hadi eneo la kuonyesha HARAKA
na ushtue hadi injini iwake. 
Onyo
 HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi
ya sumu ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika chache. HUWEZI kuiona,
kuinusa wala kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafukizo yanayotolewa, bado
unaweza kuvuta gesi ya monoksidi ya kaboni. Iwapo utaanza kuhisi mgonjwa,
kisunzi , au mchovu wakati unatumia bidhaa hii, izime na uende eneo lenye
hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa umeathiriwa na sumu
ya kaboni monoksidi. 
• Tumia bidhaa hii NJE PEKEE mbali na madirisha, milango na matundu ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi kukusanyika na uwezekano wa
kuwa inasambazwa kuelekea maeneo ya nje. 
• Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi ya kaboni vinavyotumia
betri pamoja na hifadhi ya betri kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Ving'ora
vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi. 
• USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya
ardhi, ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia
viyoyozi ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Gesi ya kaboni
monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika maeneo haya na inaweza
kukwama kwa saa kadhaa, hata baada ya bidhaa hii kuzimwa. 
• KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unatelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu. 
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Kabla ya kuwasha injini,
hakikisha umeongeza oili kulingana na maelekezo yaliyo kwenye mwongozo huu.
Iwapo utawasha injini bila mafuta, itaharibika hadi kushindwa kukarabatiwa na
hutafidiwa chini ya udhamini huu. 
Kumbuka: Kifaa kinaweza kuwa na vidhibiti mbali. Tazama mwongozo wa kifaa kwa
utambuzi na uendeshaji wa vidhibiti mbali. 
1.
Kagua oili ya injini. Tazama sehemu ya Kuangalia Kiwango  cha Oili. 
2.
Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa. 
3.
Songeza kidhibiti injini / TransportGuard® (A, Kielelezo 16) hadi eneo la
HARAKA au ENDESHA. Endesha injini kidhibiti kikiwa katika eneo la kuonyesha
HARAKA au ENDESHA.
4.
Songeza kidhibiti choki (B, Kielelezo 16) hadi eneo la IMEFUNGWA.
Kumbuka: Kwa kawaida choki haihitajiki wakati wa kuwasha injini iliyo na joto. 
5.
Rudisha Nyuma Kianzishaji, ikiwa kipo: Kwa uthabiti shikilia sehemu ya
kushika ya kamba ya kianzishaji (C, Kielelezo 16). Vuta kamba ya kianzishi
polepole hadi uhisi upinzani, kisha vuta haraka.
Onyo
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishi (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Inaweza kupelekea mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Wakati wa
kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi inakuwa gumu kuvuta
na kisha uvute kwa haraka ili kuzuia kuvutwa nyuma kwa haraka. 
6.
Swichi ya Kianzishaji cha Umeme, ikiwa ipo: Songeza swichi ya kianzishaji
kwa umeme (D, Kielelezo 16) hadi eneo la ANZA (START).
Notisi
Ili kurefusha maisha ya kianzishi, tumia misururu mifupi ya kuanzisha
(upeo wa sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko ya kuanzisha. 
7.
Injini inaposhika joto, songeza kidhibiti choki (B, Kielelezo 16) hadi kwenye eneo
la FUNGUA.
Kumbuka: Iwapo injini haitaanza baada ya majaribio ya kurudia, wasiliana na mtoa
huduma wako wa ndani au nenda kwenye VanguardPower.com au piga simu
1-800-999-9333 (Marekani). 
Simamisha Injini
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana. 
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo. 
• Ujaribu kutoruhusu hewa kuingia kwenye kabureta ili kusimamisha injini. 
Kidhibiti Injini / TransportGuard®: Songeza kidhibiti injini / TransportGuard® (A,
Kielelezo 16) hadi eneo la ZIMA au SIMAMA. 
Kumbuka: Wakati kidhibiti injini / TransportGuard® ipo katika eneo la ZIMA au SIMAMA,
vali ya mafuta itakuwa katika eneo la ZIMA. Kila wakati songeza kidhibiti injini /
TransportGuard® hadi kwenye eneo la ZIMA au SIMAMA wakati unaposafirisha kifaa. 
49

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

Vanguard 12v000

Table of Contents