Briggs & Stratton 131D000 Operator's Manual page 45

Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Kagua kiwango cha oili ya injini.
Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla au ekzosi na vidhibiti.
Kagua kisafishaji hewa.
Mpishano wa Saa 100 au Kila Mwaka
Badilisha oili ya injini.
Kagua oili na usafishe chujio za mafuta.
Safisha mapezi ya kupoesha oili
Kila Mwaka
Badilisha chujio za hewa.
Badilisha chujio la mafuta.
Safisha mfumo wa kupoesha hewa
1
Safisha mara nyingi zaidi katika mazingira ya vumbi au wakati kuna vipengee vingi
hewani.
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafukizo
ONYO 
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Vitu vinavyoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi, vinaweza kushika
moto.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442, kutumia
au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi, au
lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama ilivyobainishwa katika
sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka nyingine
za majimbo au serikali ya kitaifa huenda zikawa na sheria sawia; Rejelea Kanuni za
Serikali ya KItaifa ya 36 CFR Sehemu ya 261.52. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa
kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya
mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
Ondoa vifuzi vilivyokusanyika kutoka kwenye mafla na eneo la silinda. Kagua mafla
kama ina nyufa, ubabuzi, au uharibifu mwingine. Ondoa kifaa cha kusonga au kishika
cheche, iwapo kipo, na ukague kama kuna uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Iwapo
uharibifu utapatikana, sakinisha sehemu za ubadilishaji kabla ya kuendesha kifaa.
ONYO 
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo sawa
kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au kusababisha
majeraha.
Badilisha Oili ya Injini
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la
mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto
au mlipuko.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa njia sahihi. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma
au muuzaji ili kupata zana salama za kutupa au kutumia tena.
Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa IMEZIMWA lakini bado ina joto, ondoa ufunguo kwenye swichi ya
ufunguo (ikiwa upo).
2.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwaga oili (A, Kielelezo 6). Mwaga oili katika
kontena iliyoidhinishwa.
3.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (A, Kielelezo 6).
4.
Kwa miundo iliyo na chujio la oili ondoa bizimu zilizofunga chujio la oili (B, Kielelezo
7). Kisha, ondoa chujio la oili (C).
5.
Safisha chujio la oili (C, Kielelezo 7) ukitumia mafuta taa au dizeli ili kuondoa
uchafu. Ikiwa chujio la oili limeharibika, libadilishe.
1
.
1
.
6.
Sakinisha chujio la oili (C, Kielelezo7) na ukaze bizimu za kufunga chujio la oili (B).
Ongeza Oili
Hakikisha injini inadumisha mizani.
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 8). Futa oili kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili ukitumia kitambaa safi.
2.
Polepole weka oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo 8). Usijaze
kupita kiasi.  Subiri dakika moja, na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 8).
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 8) kwenye kifaa cha kupima
kiwango cha oili.
5.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 8).
Badilisha Oili katika Kifaa cha Upunguzaji
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la
mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto
au mlipuko.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa njia sahihi. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma
au muuzaji ili kupata zana salama za kutupa/kutumia tena.
1.
Ondoa kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 9).
2.
Injini ikiwa IMEZIMWA lakini ina joto, ondoa kifuniko cha tundu la kumwaga oili (B,
Kielelezo 10). Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
KUMBUKA: Vifuniko vyote vya matundu ya kumwaga oili vinaweza kuwekwa kwenye
injini.
3.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (B, Kielelezo 10).
4.
Hakikisha injini inadumisha mizani. Safisha eneo la kujazia oili (C, Kielelezo 9) na
uondoe vifusi vyote.
5.
Mwaga polepole oili ya kulainisha gia ndani ya tundu la kujazia oili (C, Kielelezo 9)
mpaka oili itokee kwenye tundu la kumwaga oili (D, Kielelezo 10). Tazama sehemu
ya Vipimo ili kujua kiwago cha oili.
6.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 9).
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa
ONYO 
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
NOTISI 
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza
kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako
na ushughulikie kama ifuatavyo.
Chujio la Hewa la Karatasi
1.
Legeza au uondoe vifaa vya kufunga, iwapo zipo, (A, Kielelezo 11).
2.
Fungua au uondoe kifuniko (B, Kielelezo 11).
3.
Ili kuzia uchafu unaoanguka kwenye kabureta, kwa makini ondoa kishajishai cha
mwanzo (D, Kielelezo 11) na chujio (C) kutoka kwenye eneo la chini la chujio la
hewa.
4.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 11), ikiwa kipo, kwenye chujio (C).
5.
Ili kulegeza vifusi, gongesha chujio (C, Kielelezo 11) kwa utaratibu kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu sana, badilisha kwa chujio jipya.
45

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

181d000261d000

Table of Contents