Briggs & Stratton 131D000 Operator's Manual page 44

Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapowasha injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji
hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la
IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi
kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
ONYO 
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu. Ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na mbali
na madirisha, milango na matundu.
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
KUMBUKA: Kifaa chako kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Rejelea mwongozo wa
kifaa ili utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia.
1.
Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kagua na Ongeza Kiwango cha Oili.
2.
Hakikisha kwamba vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Songeza kizima mafuta (A, Kielelezo 5) hadi eneo linaloonyesha FUNGUA.
4.
Songeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 5) hadi kwenye eneo linaloonyesha ANZISHA.
Endesha injini katika eneo hilo la ANZISHA.
5.
Vuta kamba ya kianzishaji (C, Kielelezo 5) polepole hadi uhisi inakuwa gumu
kuvuta.
6.
Zungusha kamba ya kianzishaji (D, Kielelezo 5) kwenye kapi kwa mwelekeo
ulioonyeshwa na mshale. Vuta kamba ya kianzishaji (C) hadi uhisi inakuwa gumu
kuvuta.
7.
Sukuma chini kabisa wenzo wa shinikizo (E, Kielelezo 5).
8.
Vuta kianzishaji kwa haraka.
44
9.
Geuza ufunguo wa swichi (F, Kielelezo 5) (ikiwa upo) hadi eneo linaloonyesha
ANZISHA.
 Injini ikikosa kuwasha baada ya majaribio 2 au 3, wasiliana na muuzaji wako wa
ndani au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au upige simu kwa nambari
1-800-444-7774.
 Hakikisha kwamba betri imeunganishwa vizuri kabla ya kuanzisha injini. Rejelea
sehemu ya Uunganishaji Betri na Vipengele na Vidhibiti.
 Ili kurefusha maisha ya kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo wa
sekunde 5). Subiri dakika moja kati ya mizunguko ya kuanzisha.
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo kuteguka.
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
Zima Injini
1.
Songeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 5) hadi eneo linaloonyesha SIMAMA.
2.
Baada ya injini kusimama, songeza sehemu ya kufunga mafuta (A, Kielelezo 5),
hadi eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
Udumishaji
Maelezo ya Udumishaji
ONYO 
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi la
mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi ya spaki
uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au
mlipuko. Ikiwa injini imeinama katika mkao tofauti, haitaguruma kwa urahisi kwa sababu
ya kuchafuka kwa chujio la hewa au plagi ya spaki kwa oili au mafuta.
Tunapendekeza kwamba umwone Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa yeyote wa Briggs &
Stratton ili kupata huduma zote ya udumishaji na kufanyia huduma injini na sehemu za
injini.
NOTISI 
Vijenzi vyote vilivyotumiwa kutengeneza injini hii ni lazima visalie kwenye maeneo yake
ili kupata uendeshaji bora.
ONYO 
Mwako wa injini usiokusudiwa unaweza kusababisha mshutuko wa umeme au
moto na kupelekea kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha
mabaya ya ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
Tenganisha waya wa plagi ya spaki na uuweke mbali na plagi ya spaki.
Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishaji cha umeme.)
Tumia zana sahihi pekee.
Unapokagua uwepo wa cheche:
Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Ili kupata huduma ya udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo
ya kudhibiti mafukizo, wasiliana na kituo chochote kinachohitimu cha kukarabati
injini au mtoa huduma aliyehitimu wa kukarabati injini. Hata hivyo, ili kupata
huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na muuzaji
aliyeidhinishwa na kiwanda. Rejelea Kauli za Udhibiti Mafukizo.
Ratiba ya Udumishaji
Saa 20 za Kwanza
Badilisha oili ya injini.
Safisha chujio la oili.
Mpishano wa Saa 8 au Kila Siku
BRIGGSandSTRATTON.COM

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

181d000261d000

Table of Contents