Briggs & Stratton 131D000 Operator's Manual page 43

Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Kiwango cha Mafuta -
Upeo
Usijaze Kupita Kiasi
Uendeshaji
Mapendekezo ya Oili
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
Kiwango cha Oili: Tazama sehemu ya Vipimo.
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na Waranti ya Briggs & Stratton
kupata utendakazi bora. Oili nyingine za usafishaji zinakubalika ikiwa zimeainishwa kwa
huduma ya CK-4, CJ-4, CI-4, CH-4 au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum. 
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya nje inayotarajiwa.
A
SAE 30 - Chini ya 40 °F (4 °C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa
kuwasha.
B
10W-30 - Juu ya 80 °F (27 °C) matumizi ya 10W-30 yanaweza kusababisha
ongezeko la matumizi ya oili. Kagua kiwango cha oili mara nyingi.
C
5W-30
D
Sinthetiki 5W-30
E
®
Vanguard
 Synthetic 15W-50
Kagua Kiwango cha Oili
Kabla ya kukagua au kuongeza oili
Hakikisha injini inadumisha mizani.
Safisha vifusi kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 3) na upanguze kwa
kitambaa safi.
2.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 3).
3.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Hakikisha kwamba
kiwango cha oili kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 3) kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili.
4.
Iwapo kiwango cha oili kiko chini, polepole weka oili kwenye eneo la kujazia oili ya
injini (C, Kielelezo 3). Usiongoze oili nyingi kupita kiasi.
5.
Subiri dakika moja na ukague tena kiwango cha oili. Hakikisha kwamba kiwango
cha oili ni sahihi.
6.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 3).
Mfumo wa Ulinzi dhidi ya Oili Chache (iwapo upo)
Kihisio cha oili chache kimesakinishwa kwenye baadhi ya injini. Iwapo oili iko chini,
kihisio kitaonyesha mwangaza wa onyo au kuzima injini. Zima injini na ufuate hatua
zifuatazo kabla ya kuwasha injini.
Hakikisha injini haijainama.
Kagua kiwango cha oili. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
Iwapo kiwango cha oili kiko chini, ongeza kiwango sahihi cha oili. Washa injini
na uhakikishe kwamba mwangaza wa onyo (iwapo upo) hauwashi.
Iwapo kiwango cha oili hakiko chini, usiwashe injini. Wasiliana na Muuzaji
Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kurekebisha tatizo hilo la oili.
Mapendekezo ya Mafuta
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
Vipimo Maalum vya Mafuta ya Dizeli
ASTM D975
No. 1-D S15
No. 2-D S15
EN 590
ISO 8217 DMX
JIS K2204 Grade No. 2
®
ili
KSM-2610
Tumia tu mafuta mapya ya dizeli.
Nunua kwa viwango vinavyoweza kutumika ndani ya siku 180 ili kuhakikisha
kwamba mafuta ni mapya.
Tumia mafuta ya dizeli ya msimu wa kiangazi (No. 2D) katika joto linalozidi nyuzi -7°C
(20°F) na mafuta ya msimu wa baridi (No. 1-D au No. 1-D/2-D) chini ya joto hilo.
KUMBUKA: Matumizi ya mafuta ya msimu wa baridi katika joto la chini kunawezesha
utiririkaji wakati wa baridi, jambo ambalo linarahisisha kuwasha na kupunguza kuzibika
kwa chuji la mafuta.
Kutumia mafuta ya msimu wa kiangazi katika joto linalozidi -7°C (20°F) kunasaidia
kurefusha maisha ya pampu ya mafuta na nguvu nyingi ikilinganishwa na mafuta ya
msimu wa baridi.
TAHADHARI Usitumie mafuta ya dizeli ambayo hayajaidhinishwa. Usichanganye oili
kwenye dizeli au kurekebisha injini ili itumie mafuta mbadala. Ukitumia mafuta ambayo
hayajaidhinishwa kutaharibu vijenzi vya injini na ifanye waranti ya injini kuwa batili.
Ongeza Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapoongeza mafuta
Zima injini. Kabla ya kufunua kifuniko, subiri angalau dakika mbili (2) ili
kuhakikisha injini imepoa.
Jaza tangi la mafuta ukiwa nje au katika eneo lenye hewa nyingi safi.
Usiweke mafuta mengi kupita kiasi kwenye tangi. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
1.
Safisha kifuniko cha mafuta kutokana na uchafu na vifusi. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la mafuta (A, Kielelezo 4) kwa mafuta. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze zaidi ya chini mwa shingo ya tangi la mafuta (B).
3.
Weka kifuniko cha mafuta.
Washa Injini
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo kuteguka.
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
Eneo
USA
European Union
Kimataifa
Japani
Korea
43

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

181d000261d000

Table of Contents