Briggs & Stratton Vanguard 10V000 Operator's Manual page 57

Hide thumbs Also See for Vanguard 10V000:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Maelezo Jumla
Mwongozo huu una maelezo ya usalama ili kukufahamisha kuhusu hatari zinazohusiana
na injini hizi na jinsi ya kuzizuia. Pia una maagizo ya matumizi na udumishaj mwema
wa injini. Kwa sababu Briggs & Stratton haijui hususan injini hii itaendesha kifaa kipi,
ni muhimu kwamba usome, uelewe na utii maagizo haya. Hifadhi maagizo haya asili
kwa marejeleo ya siku zijazo.
KUMBUKA: Vielelezo na mifano iliyo katika mwongozo huu ni ya marejeleo pekee na
huenda ikatofautiana na muundo wako. Ikiwa unahitaji usaidizi, wasiliana na Muuzaji
Huduma Aliyeidhinishwa.
Kwa vipuri vya kubadilishia au usaidizi wa kiufundi, rekodi hapa chini muundo, aina,
na nambari za msimbo za injini. Nambari hizi zinapatikana kwenye injini yako. Rejelea
sehemu ya Vipengele na Vidhibiti.
Tarehe ya Ununuzi
Muundo wa Injini - Aina - Msimbo
Nambari Tambulishi ya Injini
Maelezo ya Mawasiliano ya Ofisi ya Ulaya
Ukiwa na maswali kuhusiana na mafukizo ya Ulaya, wasiliana na ofisi yetu ya Ulaya
kupitia:
Max-Born-Straße 2, 68519 Viernheim, Germany. 
Umoja wa Ulaya (EU) Awamu ya V (5):
Viwango vya Kaboni Dioksidi (CO2)
Andika CO2 ndani ya upau wa kutafuta kwenye BriggsandStratton.com ili kupata
viwango vya kaboni dioksidi vya injini za Briggs & Stratton zilizoidhinishwa za Aina ya
EU. 
Utumiaji tena wa Taarifa
Tumia tena mifuko yote, maboksi, oili na betri zilizotumika
kama ilivyobainishwa na kanuni za serikali.
Usalama wa Mwendeshaji
Ishara ya Tahadhari ya Usalama na Maneno ya
Ishara
Alama ya tahadhari ya kiusalama ya
kuhusu hatari zinazoweza kusababisha jeraha la kibinafsi. Neno la ishara (HATARI,
ONYO, au TAHADHARI) linatumika kuonyesha uwezekano wa kujeruhiwa na ubaya
wa jeraha hilo. Kwa kuongezea, alama ya hatari inatumika kuwakilisha aina ya hatari.
HATARI inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa, itasababisha kifo au jeraha
mbaya sana.
ONYO inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa, inaweza kusababisha kifo au jeraha
mbaya sana.
TAHADHARI inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa, inaweza kusababisha jeraha
dogo au wastani.
ILANI inaonyesha maelezo yanayozingatiwa kuwa muhimu, lakini hayahusiani na
hatari.
Alama za Hatari na Maana Yake
Maelezo ya usalama
kuhusu hatari zinazoweza
kusababisha jeraha la
kibinafsi.
Hatari ya Moto
Hatari ya Mshtuko
inatambulisha maelezo ya usalama
Soma na uelewe
Mwongozo wa
Mwendeshaji kabla ya
kutumia kifaa au kukifanyia
huduma.
Hatari ya Mlipuko
Hatari ya Moshi wenye
Sumu
Hatari ya Maeneo Moto
Hatari ya Vitu
Vinavyorushwa - Vaa vifaa
vya kukinga macho.
Hatari ya Jamidi
Hatari ya Kukatwa Viungo -
Sehemu Zinazosonga
Hatari ya Kuchomeka
Ujumbe wa Usalama
ONYO 
Injini za Briggs & Stratton® hazijaundwa kuzalisha nguvu za umeme au kuendesha:
vijigari vya kufurahia; vijigari vya kuendesha; vya watoto, burudani, au magari ya
barabara ya aina yote (ATVs); pikipiki; gari la kuendeshea juu ya maji;bidhaa za ndege;
au magari yaliyotumiwa katika matukio ya mashindano yasiyowekewa vikwazo na
Briggs & Stratton. Kwa maelezo kuhusu bidhaa za mashindano ya uendeshaji magari,
tazama www.briggsracing.com. Kwa matumizi pamoja na vifaa na ATV za upande
kwa upande, tafadhali wasiliana na Kituo cha Matumizi ya Injini cha Briggs & Stratton,
1-866-927-3349. Matumizi ya injini isivyofaa inaweza kusababisha majeraha mabaya au
kifo.
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapoongeza mafuta
Zima injini. Kabla ya kufunua kifuniko, subiri angalau dakika mbili (2) ili
kuhakikisha injini imepoa.
Jaza tangi la mafuta ukiwa nje au katika eneo lenye hewa nyingi safi.
Usiweke mafuta mengi kupita kiasi kwenye tangi. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
Unapowasha injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji
hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la
IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi
kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
Unapoendesha kifaa
Usiinamishe injini au kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
Usikabe kabureta (iwapo ipo) ili kusimamisha injini.
Usiwashe au kuendesha injini kamwe wakati kisafishaji hewa (iwapo kipo) au
chujio la hewa (iwapo lipo) vimeondolewa.
Unapofanyia huduma ya udumishaji
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la
mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto
au mlipuko.
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi
la mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi
ya spaki uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na
kusababisha moto au mlipuko.
Hatari ya Kelele - Ulinzi wa
masikio unapendekezwa
kwa matumizi ya muda
mrefu.
Hatari ya Mlipuko
Hatari ya Kuvutwa Nyuma
kwa Haraka
Hati ya Kemikali
Hatari ya Ubabuzi
57

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

Vanguard 12v000

Table of Contents