Briggs & Stratton 400000 Operator's Manual page 46

Hide thumbs Also See for 400000:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Shughulikia Mfumo wa Eneo la kutolea
moshi
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa
moto zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi n.k. unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
• Ni ukiukaji wa Msimbo wa Rasilimali wa Umma wa California, Sehemu ya 4442,
kutumia au kuendesha injini katika eneo linazungukwa na msitu, lililozungukwa na
brashi, au lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa eneo la kutolea moshi una kishika
cheche, kama ilivyofafanuliwa kwenye Sehemu ya 4442, iliyodumishwa kwenye
mpangilio wenye ufanisi wa kufanya kazi. Mamlaka mengine ya Majimbo au
shirikisho yanaweza kuwa sheria sawa. Wasiliana na mtengenezaji wa kifaa asili,
muuzaji wa rejareja, au mtoa huduma ili kupata kishika cheche kilichobuniwa kwa
mfumo wa eneo la kutolea moshi uliosakinishwa kwenye injini hii.
Sehemu za mfumo za kutoa moshi zinasakinishwa na mtengenezaji wa kifaa. Kwa
maelezo mahususi ya ukarabati na sehemu za kubadilisha, wasiliana na mtengenezaji
wa kifaa.
Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye mafla na eneo la silinda. Kagua mafla kwa
nyufa, kutia kutu, au uharibifu mwingine. Ondoa kifaa cha kusonga au kishika cheche,
iwapo kipo, na ukague kwa uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Iwapo uaribifu utapatikana,
sakinisha sehemu za ubadilishaji kabla ya kuendesha.
Onyo
Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa katika eneo sawa
kama sehemu asili. Sehemu zingine huenda zisitekeleze vilevile, zinaweza kuharibu
kitengo, na inaweza kusababisha majeraha.
Badilisha Mafuta ya Injini
Tazama Kelelezo: 7, 8, 9, 10
Mafuta yaliyotumiwa ni bidhaa taka yenye madhara na lazima itupwe vizuri. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha usaidizi
au mtoa huduma kwa utupaji/kutumia upya salama kwa bidhaa.
Ondoa Mafuta
1.
Injini ikiwa bado ina joto, tenganisha waya wa kiziba cheche (D, Kielelezo 7) na
uihifadhi mbali na kiziba cheche (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta (A, Kielelezo 8).
Kiziba cha Kitoaji Mafuta, iwapo kipo
1.
Ondoa kiziba cha kutoa mafuta (F, Kielelezo 8). Weka mafuta kwenye kontena
iliyoidhinishwa.
Kumbuka: Viziba cheche mbalimbali vya kutoa mafuta (G, Kielelezo 8) vimesakinishwa.
2.
Baada ya mafuta kutolewa, sakinisha na ukaze kiziba cha kutoa mafuta (F,
Kielelezo 8).
Kitoaji Mafuta cha Haraka, iwapo kipo
1.
Ondoa bomba la kutoa mafuta haraka (H, Kielelezo 9) kutoka upande wa injini.
2.
Geuza na uondoe kifuniko cha kutoa mafuta (I, Kielelezo 9). Teremsha kitoa
mafuta haraka kwa utaratibu (H) katika kontena iliyoidhinishwa (J).
3.
Baada ya mafuta kutolewa, sakinisha kifuniko cha kutoa mafuta haraka (I,
Kielelezo 9). Ambatisha bomba la kutoa mafuta haraka (H) kwenye upande wa
injini.
Badilisha Kichujio cha Mafuta, iwapo kipo
Baadhi ya modeli zina kichujio cha mafuta. Kwa vipindi vya ubadilishaji, tazama Ratiba
ya Udumishaji.
1.
Toa mafuta kutoka kwenye injini. Tazama eneo la Kuondoa Mafuta .
2.
Ondoa kichujio cha mafuta (K, Kielelezo 10) na ukitupe vizuri.
3.
Kabla usakinishe kichujio kipya cha mafuta, lainisha kiasi kwa kifaa cha kichujio
cha mafuta kwa mafuta freshi na safi.
4.
Sakinisha kichujio cha mafuta kwa mkono hadi kifaa kisgusane na adapta ya
kichujio cha mafuta, kisha kaza kichujuio cha mafuta kwa mizunguko 1/2 hadi 3/4.
46
5.
Ongeza mafuta. Tazama sehemu Ongeza Mafuta .
6.
Washa na uendeshe injini. Wakati injini inachemka, angali uvujaji wa mafuta.
7.
Zima injini na uangalie kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha mafuta kiko juu
ya kiashiria kilichojaa (B, Kielelezo 8) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha
mafuta.
Ongeza Mafuta
• Hakikisha kuwa mtambo uko katika kiwango.
• Safisha eneo la kujaza mafuta kutokana na uchafu wowote.
• Tazama Vipimo katika eneo la kiwango cha mafuta.
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 8) na upanguse kwa
kitambaa safi.
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la injini (C, Kielelezo 8).
Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza mafuta, subiri dakika moja na kisha
angalia kiwango cha mafuta.
Kumbuka: Usiongeze mafuta kwenye kitoaji mafuta cha haraka (H, Kielelezo 9) iwapo
kipo.
3.
Sakinisha na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 8).
4.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta na ukague kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi
cha mafuta kiko juu ya kiashiria kilichojaa (B, Kielelezo 8) kwenye kifaa cha
kuangalia kiwango cha mafuta.
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 8).
6.
Unganisha waya wa kuziba cheche (D, Kielezo 7) kwenye kuziba cheche (E).
Shughulikia Kichuja Hewa
Tazama Kelelezo: 11, 12, 13
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
• Kamwe usiwashe na kuendesha wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo
kipo) au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Modeli mbalimbali aidha zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia
zinaweza kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na
kutumiwa tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye
injini yako na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 11).
2.
Ondoa kifuniko cha kichujio cha hewa (B, Kielelezo, 11).
3.
Ondoa kichujio (C, Kielelezo 11) na kisafishaji cha mwanzo (D), iwapo kipo.
4.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio katika eneo gumu. Iwapo kichujio
ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
5.
Osha kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 11), iwapo kipo, kwenye sabuni oevu
na maji. Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta
kwenye kisafishaji cha mwanzo.
6.
Kusanya kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 11), iwapo kipo, na kichujio (C)
katika sehemu ya chini ya kichujio cha hewa (E).
7.
Sakinisha kifuniko cha kichujio cha hewa (B, Kielelezo 11) na ulinde kwa bizimu
(A). Hakikisha bizimu imekazwa.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 12, 13).
2.
Ondoa kifuniko cha kichujio cha hewa (B, Kielelezo 12, 13).
3.
Ili kuondoa kichujio (C, Kielelezo 12, 13), nyanyua mwisho wa kichujio.
4.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio katika eneo gumu. Iwapo kichujio
ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
5.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 12, 13), ikiwa kipo, kwenye kichujio
(C).
6.
Osha kisafishaji cha mwanzo (C, Kielelezo 12, 13), iwapo kipo, kwenye sabuni
oevu na maji. Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta
kwenye kisafishaji cha mwanzo.
BRIGGSandSTRATTON.com

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

490000440000

Table of Contents