Snapper SPX-100 Operator's Manual page 111

Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Chaguo ya Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma
(RMO)
ONYO
Ukataji nyasi ukirudi nyuma unaweza kuwa hatari kwa
watazamaji. Ajali za kuhuzunisha zinaweza kutokea
ikiwa mwendeshaji hatahadhari kuwepo kwa watoto.
Usiwahi kuwasha RMO karibu na watoto. Watoto mara
nyingi huvutiwa ka kifaa hicho na shughuli ya kukata
nyasi.
Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma (RMO) humruhusu
mwendeshaji kukata nyasi akirudi nyuma (angalia
Vipengele na Vidhibiti). Ili kuwasha, zungusha kifunguo
cha RMO baada ya kuewak PTO. Taa ya L.E.D. itaangaza,
na kisha mwendeshaji anaweza kukata nyasi akirudi nyuma.
Kila wakati PTO imewekwa RMO inahitaji kuwashwa upya
ikiwa unataka. Kifunguo kinadaa kuondolewa ili uzuie ufikiaji
wa RMO.
Kusukuma Trekta kwa Mikono
1 Toa PTO na uzime injini.
2 Vuruta ubadilishaji gia (A, Mchoro 7) nyuma angalau
2-3/8" (6 cm) ili ufunge upande wa kuwachilia.
3 Trekta sasa inaweza kusukumwa kwa mikono.
ONYO
Kuvuta kifaa kutasababisha uharibifu wa klachi na
gea. Usitumie gari jengine kusukuma au kuvuta kifaa.
Usianzishe wenzo wa kubadilisha gia wakati injini
imewashwa.
Kurekebisha Urefu wa Kukata Nyasi
Tumia wenzo wa kurekebisha urefu wa kukata nyasu kuinua
au kuteremsha urefu wa kikata (angalia Vipengele na
Vidhibiti).
Urefu wa kukata una nafasi saba katik ya 1.5" na 4.0" (3,8 na
10,2 cm).
Mita ya Saa (ikiwa kunayo)
Mita ya Saa huonyesha jumla ya saa, saa za safari, na saa
dijitali. Angalia Mchoro 8 kwa uonyesho la Mita ya Saa.
Onyesha Jumla ya Saa, Saa za Safari, na Saa
KUMBUKA: Wakati unawasha kifaa, Jumla ya Saa
inaonekana. Jumla ya saa itawekwa upya kiotomatiki kwa 0
baada ya 999.9.
1. Bonyeza MODI kwa chini ya sekunde 1 ili uone Saa za
Safari.
2. Bonyeza WEKA UPYA kwa zaidi ya sekunde 3 ili uweke
upya Saa za Safari kuwa 0.
3. Bonyeza MODI kwa chini ya sekunde 1 ili uone Saa
(angalia fungu la Weka Saa).
4. Bonyeza MODI kwa chini ya sekunde 1 ili urudi kwenye
Jumla ya Saa.
Weka Saa
1. Bonyeza MODI kwa zaidi ya sekunde 3. Saa zitaonekana
kwenye onyesho.
2. Bonyeza WEKA UPYA ili urekebishe saa.
3. Bonyeza MODI kwa chini ya sekunde 1 ili uhifadhi
mpangilio. Dakika zitaonekana kwenye onyesho.
4. Bonyeza WEKA UPYA ili urekebishe dakika.
5. Bonyeza MODI kwa chini ya sekunde 1 ili uhifadhi
mpangilio.
Breki ya Kuegesha
Tumia udhibiti wa breki ya kuegesha kuweka au kutoa breki
ya kuegesha wakati trekta imezimamishwa (Vipengele na
Vidhibiti).
Weka Breki ya Kiegesha - Ili uweke breki ya kuegesga,
kanyaga pedali ya breki kabisa, vuruta JUU kidhibiti cha
breki ya kuegesha, na uwachilie pedali ya breki.
Toa Breki ya Kuegesha - Ili utoe breki ya kuegesha,
kanyaka pedali ya breki kabisa, bonyeza CHINI kidhibiti cha
breki ya kuegesha, na uwachilie pedali ya breki.
Udhibiti wa Uendaji kwa Kadiri
KUWEKA:
1 Kanyaga pedali ya kuenda mbele (angalia Vipengele na
Vidhibiti).
2 Inua udhibiti wa uendaji kwa kadiri wakati kasi unayotaka
imefikiwa. Uendaji kwa kadiri utafunga katika moja ya
sehemu zake tano za kufunga.
KUTOA:
1 Bonyeza pedali ya breki.
AU
2 Kanyaga pedali ya kuenda mbele.
Kusimamisha Trekta na Injini
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto
haraka sana na kulipuka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha
mabaya ya moto au kifo.
• Usichoki kabureta kuzima injini.
1 Wachilia pedali za kuenda mbele ili urudi kwa sehemu ya
GIA HURU (angalia Vipengele na Vidhibiti).
2 Ukiwa bado kwenye nyasi, toa swichi ya PTO, kisha
usubiri sehemu zote zinazosonga zisimame.
3 Sogeza udhibiti wa kifaa cha kudhibiti mmiminiko wa
mafuta (au udhibiti wa mmiminiko wa mafuta/choki) kwa
sehemu ya mwendo wa POLEPOLE na UZIME kifunguo
cha kuwasha. Ondoa Ufunguo.
4 Weka breki ya kuegesha. Kanyaga breki ya kuegesha
kabisa, vuruta JUU kidhibiti cha breki ya kuegesha, na
uwachilie pedali ya breki.
Katika hali ya dharura injini inaweza kusimamishwa
kwa urahisi kwa kuzungusha switchi ya kuwashia
kwenye SIMAMA.
sw
11

Hide quick links:

Advertisement

Table of Contents
loading

Table of Contents