Snapper SPX-100 Operator's Manual page 109

Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Angalia au Ongeza Oili
Kabla ya kuongeza au kuangalia oili
• Weka trekta kwenye eneo tambarare (angalia Mchoro 4).
• Ondoa vifusi vyovyote kutoka eneo la tangi la oili.
1 Ondoa kijiti cha kupimia oili (A, Mchoro 5) na ukipanguse
na kitambaa safi.
2 Ingiza na ukaze kijiti cha kupimia oili.
3 Ondoa kijiti cha kupimia oili na uangalie kiwango cha oili.
Inafaa iwe katika alama ya KAMILI (B) kwenye kijiti cha
kupimia oili.
4 Ikiwa chini, ongeza oili polepole ndani ya kopo la oili ya
injini (C). Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza oili,
subiri dakika moja na kisha uangalie kiwango cha oili
tena.
KUMBUKA: Usiongeze oili katika bomba la oili la haraka
(ikiwa kunalo).
5 Regesha na ukaze kijiti cha kupimia oili.
Shinikizo la Oili
Ikiwa shinikizo la oili liko chini sana, swichi ya shinikizo
(ikiwa kunayo) itazima injini au kuwasha kifaa cha onyo
kwenye kifaa. Jambo hili likifanyika, zima injini na uangalie
kiwango cha oili ukitumia kijiti cha kupimia oili.
Ikiwa kiwango cha oili kiko chini ya alama ya ONGEZA,
ongeza oili hadi ifike alama ya JAA. Washa injini na ukague
shinikizo linalofaa kabla ya kuendelea kuendesha.
Ikiwa kiwango cha oili kiko kati ya alama za ONGEZA na
JAA, usiwashe injini. Wasiliana na muuzaji aliyeidhinishwa
kusawazisha matatizo ya shinikizo la oili.
Mapendekezo ya Mafuta
Lazima mafuta yatimize mahitaji haya:
• Petroli safi, mpya, isiyo na ledi.
• Oktani ya kiwango cha chini cha 87/87 AKI (91 RON).
Matumizi ya mwinuko wa juu, angalia hapa chini.
• Petroli iliyo na ethanoli ya 10% (gesiholi) inakubalika.
ILANI: Usitumie petroli ambazo hazijaidhinishwa, kama vile
E15 na E85. Usichanganye oili katika petroli au kubadilisha
injini ili itumie mafuta mbadala. Ukitumia mafuta ambayo
hayajaidhinishwa kutaharibu vijenzi vya injini na ifanye
dhamana ya injini kuwa batili.
Ili kulinda mfumo wa mauta kutokana na utokeaji wa gundi,
changanya kisawazisha mafuta katika mafuta. Angalia
Uwekaji. Mafuta yote ni tofauti. Ikiwa utakumbana na
matatizo ya kuwasha au utendaji, badilisha wauza mafuta
au badilisha chapa. Injini hii imeidhinishwa kuendeshwa na
petroli. Mfumo wa udhibiti utoaji moshi wa injini hii ni EM
(Marekebisho ya Injini)
Mwinuko wa Juu
Katika mwinuko zaidi ya fiti 5,000 (mita 1,524), kiwango
cha chini cha oktani ya 85//85 AKI (89 RON) cha petroli
kinakubalika. Ili uendelee kutii utoaji moshi, marekebisho ya
mwinuko wa juu yanahitajika. Uendeshaji bila urekebishaji
huu utasababisha kupungua kwa utendaji, kuongezeka
kwa matumizi ya mafuta, na kuongezeka kwa utoaji ekzosi.
Mtembelee Muuzaji aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton
kwa taarifa ya urekebishaji wa mwinuko wa juu.
Uwashaji wa injini katika miinuko chini ya fiti 2,500 (mita 762)
ikiwa na urekebishaji wa mwinuko wa juu haupendekezwe.
Kuongeza Mafuta
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto
haraka sana na kulipuka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha
mabaya ya moto au kifo.
Wakati wa Kuongeza Mafuta
• Zima injini na uwache injini ipoe kwa angalau dakika 3
kabla ya kuondoa kifuniko cha mafuta.
• Jaza tangi la mafuta nje au katika eneo lenye sehemu za
kutosha za kuingiza hewa.
• Usijaze tangi la mafuta kupindukia. Ili kuruhusu uvukizi
wa mafuta, usijaze zaidi ya chini mwa shingo ya tangi la
mafuta.
• Weka mafuta mbali na cheche, moto, taa za moto, joto,
na vyanzo vingine vya mwako.
• Kagua mifereji ya mafuta, tangi, kifuniko, na vijenzi
mara kwa mara kwa nyufa au ufujaji. Badilisha ikiwa
inahitajika.
• Mafuta yakimwagika, subiri hadi ya kakauke kabla ya
kuwasha injini.
1 Safisha uchafu na vifusi kutoka eneo la kifuniko cha
mafuta. Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Mchoro 6). Pia
angalia fungu la Vipengele na Udhibiti.
2 Jaza tangi la mafuta (B) na mafuta. Ili uruhusu uvukizi wa
mafuta, usijaze hadi juu ya chini mwa shingo ya tangi la
mafuta (C).
3 Funga kifuniko cha mafuta.
sw
9

Hide quick links:

Advertisement

Table of Contents
loading

Table of Contents