Briggs & Stratton 120000 Operator's Manual page 45

Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Mwone Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata huduma zote za
udumishaji na kufanyia huduma injini na sehemu za injini.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Ili kupata huduma ya udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo
ya kudhibiti mafukizo, wasiliana na kituo chochote kinachohitimu cha kukarabati
injini au mtoa huduma aliyehitimu wa kukarabati injini. Hata hivyo, ili kupata
huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na muuzaji
aliyeidhinishwa na kiwanda. Rejelea Kauli za Udhibiti Mafukizo.
Ratiba ya Udumishaji
Saa 5 za Kwanza
Badilisha oili (haihitajiki kwenye miundo ya Just Check & Add
Mpishano wa Saa 8
Kagua kiwango cha oili ya injini.
Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla na vidhibiti.
Safisha grili ya kuingiza hewa.
Mpishano wa Saa 50 au Kila Mwaka
1
Safisha chujio la hewa
.
Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo)
Badilisha oili ya injini (haihitajiki kwenye miundo ya Just Check & Add
Badilisha chujio la oili (iwapo lipo) (haihitajiki kwenye miundo ya Just Check &
TM
Add
).
Fanyia huduma mfumo wa ekzosi.
Mpishano wa Saa 200
1
Badilisha chujio la hewa
.
Badilisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo)
Kila Mwaka
Badilisha plagi ya/za spaki.
Badilisha chujio la hewa.
Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo).
Badilisha chujio la mafuta (iwapo lipo).
Fanyia huduma mfumo wa mafuta.
Fanyia huduma mfumo wa kupoesha
2
Kagua uwazi wa vali
.
1
Safisha mara nyingi zaidi katika mazingira ya vumbi au wakati kuna vipengee vingi
hewani.
2
Haihitajiki isipokuwa kutokee matatizo ya utendakazi wa injini.
Kabureta na Kasi ya Injini
Usihitilafiane na kabureta, springi ya kidhibiti, viunganishaji, au sehemu nyingine ili
kubadilisha kasi ya injini. Iwapo marekebisho yoyote yanahitajika, wasiliana na Mtoa
Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kufanyiwa huduma.
NOTISI 
Mtengenezaji wa kifaa hubainisha kasi ya juu zaidi ya injini kama ilivyosakinishwa
kwenye kifaa. Usizidishe kasi hii. Iwapo huna uhakika kasi ya juu zaidi ya kifaa hiki
ni ipi, au kasi ya injini iilivyopangwa tangu kiwandani, wasiliana na Muuzaji Huduma
Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata usaidizi. Kwa oparesheni salama na
sahihi ya kifaa hiki, kasi ya injini inapaswa tu kurekebishwa na mtaalamu wa huduma
aliyehitimu.
Kufanyia Huduma Ekzosi na Mifumo ya Kupoesha
ONYO 
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Vitu vinavyoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi, vinaweza kushika
moto.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442, kutumia
au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi, au
lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama ilivyobainishwa katika
TM
).
1
.
TM
).
1
.
1
.
sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka nyingine
za majimbo au serikali ya kitaifa huenda zikawa na sheria sawia; Rejelea Kanuni za
Serikali ya KItaifa ya 36 CFR Sehemu ya 261.52. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa
kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya
mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
Hii ni injini inayopoeshwa kwa kutumia hewa. Uchafu au vifusi vinaweza kuzuia mtiririko
wa hewa na kusababisha injini kuwa moto sana. Hii inapelekea utendakazi usioridhisha
na kufupisha maisha ya injini. Mapezi ya kupoesha silinda yanaweza kuwa na vifusi
ambavyo haviwezi kuondolewa bila kufungua baadhi ya shemu za injini. Hakikisha
kwamba Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton amekagua na kusafisha
mfumo wa kupoesha hewa. Rejelea Ratiba ya Udumishaji.
1.
Hakikisha kwamba hakuna vitu vinavyoweza kushika moto karibu na nyuma ya
mafla.
2.
Tumia brashi au kitambaa kavu kuondoa vifusi kwenye maeneo ya kifuniko cha
chumba cha blowa, mafla na silinda. USITUMIE maji kusafisha injini.
3.
Hakikisha viunganishaji, springi na vidhibiti ni safi.
4.
Kagua mafla kama ina nyufa, ubabuzi, au uharibifu mwingine.
5.
Ondoa kifaa cha kusonga au kishika cheche, iwapo kipo, na ukague kama kuna
uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Hakikisha kwamba unasafisha au kusakinisha vipuri
kabla ya kuendesha kifaa.
Kufanyia Huduma Plagi ya Spaki
Kagua pengo la plagi ya spaki (A, Kielelezo 9) ukitumia pamba ya waya (B). Ikiwa
inahitajika, rekebisha pengo la plagi ya spaki.  Sakinisha na ukaze plagi ya spaki kwa
kiwango sahihi. Ili kupata maelezo maalum ya pengo na kukaza, rejelea sehemu ya
Maelezo.
Badilisha Oili ya Injini
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la
mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto
au mlipuko.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa njia sahihi. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma
au muuzaji ili kupata zana salama za kutupa au kutumia tena.
Kwa miundo ya Just Check & Add
, hauhitaji kubadilisha oili. Ikiwa unahitaji
kubadilisha oili, basi fuata utaratibu ufuatao.
Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa imezimwa lakini ina joto, tenganisha waya wa plagi ya spaki (D,
Kielelezo 10) na uiweke mbali na plagi ya/za spaki (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
3.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F, Kielelezo 11). Mwaga oili katika
kontena iliyoidhinishwa.
KUMBUKA: Mojawapo wa vifuniko vya matundu ya kumwaga oili kinaweza kuwa
kwenye injini.
4.
Baada ya oili kumwagwa, weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F,
Kielelezo 11).
5.
Wakati unamwaga oili kutoka kwenye mrija wa kujazia oili wa upande wa juu (C,
Kielelezo 12), weka upande wa injini ulio na plagi ya spaki (E) ukiwa umeangalia
juu. Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
Badilisha Chujio la Oili, iwapo lipo
1.
Mwaga oili kutoka kwenye injini. Rejelea sehemu ya Kuondoa Oili.
2.
Ondoa chujio la oili (G, Kielelezo 13) na ulitupe vizuri.
3.
Kabla ya kuweka chujio jipya la oili, lainisha kiasi gasketi ya chujio la oili
ukitumia oili safi.
4.
Weka chujio la oili ukitumia mkono hadi gasketi iguse adapta ya chujio la oili, kisha
ukaze chujio la oili kwa mizunguko ya 1/2 hadi 3/4.
5.
Ongeza oili. Rejelea sehemu ya Kuongeza Oili.
6.
Washa na uendeshe injini. Injini inapochemka, kagua kama kuna uvujaji wa oili.
7.
Zima injini. Hakikisha kwamba kiwango cha oili kiko juu ya alama inayoashiria
kujaa kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili. Rejelea Kukagua na Kuongeza
Oili.
45

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

140000

Table of Contents