Briggs & Stratton 120000 Operator's Manual page 43

Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Uendeshaji
ONYO 
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Ukinusa gesi
Usiwashe injini.
Usiwashe swichi za kiumeme.
Usitumie simu katika eneo hilo.
Ondoka kwenye eneo hilo.
Wasiliana na idara ya wazima moto.
Unapoendesha kifaa
Usiinamishe injini au kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
Unapohamisha kifaa hadi eneo nyingine
Hakikisha kwamba tangi la mafuta ni TUPU au kwamba vali ya kufunga mafuta
ipo katika eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
Mapendekezo ya Oili
Kiwango cha Oili: Rejelea sehemu ya Vipimo.
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na Hakikisho la Briggs & Stratton
kupata utendakazi bora. Oili nyingine za usafishaji zinaruhusiwa ikiwa zimebainishwa
kwa huduma ya SF, SG, SH, SJ au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum.
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya nje inayotarajiwa. Injini kwenye
vifaa vingi vya kutumiwa nje zinafanya kazi vyema zikitumia oili ya 5W-30 Synthetic.
Kwa vifaa vinavyoendeshwa katika joto la juu, oili ya Vanguard
inatoa ulindaji bora.
A
SAE 30 - Chini ya 40 °F (4 °C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa
kuwasha.
B
10W-30 - Juu ya 80 °F (27 °C) matumizi ya 10W-30 yanaweza kusababisha
ongezeko la matumizi ya oili. Kagua kiwango cha oili mara nyingi.
C
5W-30
D
Sinthetiki 5W-30
E
®
Vanguard
 Synthetic 15W-50
Kagua Kiwango cha Oili
Kabla ya kukagua au kuongeza oili
Hakikisha injini inadumisha mizani.
Safisha vifusi kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5) na upanguze kwa
kitambaa safi.
2.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
3.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Hakikisha kwamba
kiwango cha oili kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 5) kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili.
4.
Iwapo kiwango cha oili kiko chini, polepole weka oili kwenye eneo la kujazia oili ya
injini (C, Kielelezo 5). Usiongoze oili nyingi kupita kiasi.
5.
Subiri dakika moja na ukague tena kiwango cha oili. Hakikisha kwamba kiwango
cha oili ni sahihi.
6.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
Mapendekezo ya Mafuta
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
NOTISI 
Usitumie petroli ambayo haijaidhinishwa, kama vile E15 na E85. Usichanganye oili
kwenye petroli au kurekebisha injini ili itumie mafuta mbadala. Matumizi ya mafuta
ambayo hayajaidhinishwa yataharibu vipengele vya injini, na haitakarabatiwa chini ya
waranti.
Ili kulinda mfumo wa mafuta kutokana na utengenezaji wa gundi, na ubabuzi,
changanya kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya ethanoli ndani ya mafuta. Rejelea
sehemu ya Uhifadhi. Mafuta yote si sawa. Iwapo matatizo ya kuwasha au utendakazi
yatatokea, badilisha unakonunua mafuta au ubadilishe aina. Injini hii imeidhinishwa
kuendeshwa kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti mafukizo wa injini za kabureta ni EM
(Engine Modifications (Marekebisho ya Injini)). Mifumo ya kudhibiti mafukizo kwa injini
zilizo na unyonyaji mafuta kielektroniki ni ECM (Engine Control Module (Moduli ya
Kidhibiti Injini)), MPI (Multi Port Injection (Unyonyaji kwa Matundu Kadhaa)) na ikiwa ina
O2S (Oxygen Sensor (Sensa ya Oksijeni)).
®
 ili
Mwinuko wa Juu
Katika minuko zaidi ya fiti 5,000 (mita 1524), kiwango cha chini cha okteni 85 / AKI 85
(RON 89) cha petroli kinakubalika.
Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika ili kudumisha
utendakazi. Uendeshaji bila marekebisho haya unaweza kusababisha kupunguka kwa
®
15W-50 Synthetic
utendakazi, matumizi ya mafuta kuongezeka, na mafukizo kuongezeka. Wasiliana na
Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kwa maelezo ya marekebisho ya
mwinuko wa juu. Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya fiti 2,500 (mita 762) na
marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uingizaji Mafuta wa Kielektroniki (EFI), hakuna marekebisho ya mwinuko
wa juu yanahitajika.
Ongeza Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapoongeza mafuta
1.
Safisha kifuniko cha mafuta kutokana na uchafu na vifusi. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la mafuta (A, Kielelezo 6) kwa mafuta. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze zaidi ya chini mwa shingo ya tangi la mafuta (B).
3.
Weka kifuniko cha mafuta.
Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded).
Kiwango cha chini zaidi cha okteni 87/AKI 87 (91 RON). Matumizi katika
mwinuko wa juu, tazama hapa chini.
Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasoholi) inaruhusiwa.
Zima injini. Kabla ya kufunua kifuniko, subiri angalau dakika mbili (2) ili
kuhakikisha injini imepoa.
Jaza tangi la mafuta ukiwa nje au katika eneo lenye hewa nyingi safi.
Usiweke mafuta mengi kupita kiasi kwenye tangi. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
43

Advertisement

Table of Contents
loading

This manual is also suitable for:

140000

Table of Contents