Briggs & Stratton 83100 Operator's Manual page 37

Hide thumbs Also See for 83100:
Table of Contents

Advertisement

Available languages
  • EN

Available languages

  • ENGLISH, page 1
Hakimili ya © Briggs & Stratton Corporation, Milwaukee, WI, Marekani. Haki zote
zimehifadhi.
Mwongozo huu una maelezo ya usalama ili kukufahamisha kuhusu hatari zinazohusiana
na injini hizi na jinsi ya kuziepuka hatari hizo. Pia una maagizo ya matumizi bora na
utunzaji mwema wa injini. Kwa sababu Shirika la Briggs & Stratton halijui hususan
injini hii itaendesha kifaa kipi, ni muhimu kwamba usome na uelewe maagizo haya na
maagizo ya kifaa. Hifadhi maagizo haya asili kwa marejeleo ya siku zijazo. 
Kumbuka: Vielelezo na mifano iliyo katika mwongozo huu imetolewa kwa marejeleo
pekee na huenda ikatofautiana na muundo wako maalum. Wasiliana na muuzaji wako
iwapo una maswali. 
Kwa vipuri vya kubadilishia au usaidizi wa kiufundi, rekodi hapa chini muundo, aina, na
nambari za msimbo za injini pamoja na tarehe ya ununuzi. Nambari hizi zinapatikana
kwenye injini yako (tazama sehemu ya  Vipengele na Udhibiti ). 
 Tarehe ya Ununuzi 
 Muundo wa Injini - Aina - Msimbo 
 Nambari Tambulishi ya Injini 
Utumiaji tena wa Taarifa
Ufungaji wote, mafuta yaliyotumika, na betri zote
zinapaswa kutumiwa upya kulinagana na kanuni za serikali
zinazotekelezwa.
Usalama wa Opareta
Ishara ya Tahadhari ya Usalama na
Maneno ya Ishara
Alama ya tahadhari ya kiusalama (
kuhusu hatari zinazoweza kusababisha jeraha la kibinafsi. Neno la ishara (HATARI,
ONYO, au TAHADHARI) linatumika pamoja na alama ya ishara ili kuonyesha
uwezekano wa kujeruhiwa na ubaya wa jeraha hilo. Kwa kuongezea, alama ya hatari
inaweza kutumika kuwakilisha aina ya hatari. 
 
  HATARI inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa, itasababisha kifo au jeraha
mbaya sana. 
 
  ONYO inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa, inaweza kusababisha kifo au
jeraha mbaya sana. 
 
  TAHADHARI inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa, inaweza kusababisha
jeraha dogo au wastani. 
 ILANI  huonyesha hali ambayo inaweza kusababisha uharibifu wa bidhaa. 
Alama za Hatari na Maana Yake
Maelezo ya usalama
kuhusu hatari zinazoweza
kusababisha jeraha la
kibinafsi. 
Hatari ya moto 
Hatari ya mshtuko 
Hatari ya maeneo moto 
hatari ya vitu
vinavyorushwa - Vaa vifaa
vya kukinga macho. 
 
) inatumika kutambulisha maelezo ya usalama
Soma na uelewe Mwongozo
wa Mwendeshaji kabla ya
kutumia kifaa au kukifanyia
huduma. 
Hatari ya mlipuko 
Hatari ya moshi wenye sumu 
Hatari ya kelele - Ulinzi wa
masikio unapendekezwa kwa
matumizi ya muda mrefu. 
Hatari ya mlipuko 
Hatari ya jamidi 
Hatari ya kukatwa viungo -
sehemu zinazosonga 
Hatari ya kuchomeka 
Ujumbe wa Usalama
Onyo
Injini za Briggs & Stratton® hazijaundwa kuzalisha nguvu za umeme au kuendesha:
vijigari vya kufurahia; vijigari vya kuendesha; vya watoto burudani, au magari ya
barabara ya aina yote (ATVs); pikipiki; gari la kuendeshea juu ya maji; bidhaa za
ndege; au magari yaliyotumiwa katika matukio ya mashindano yasiyowekewa
vikwazo na Briggs & Stratton. Kwa maelezo kuhusu bidhaa za mashindano ya
uendeshaji magari, tazama www.briggsracing.com. Kwa matumizi pamoja na vifaa na
ATV za upande kwa upande, tafadhali wasiliana na Kituo cha Matumizi ya Injini cha
Briggs & Stratton, 1-866-927-3349. Utumizi mbaya wa injini unaweza kusababaisha
majeraha mabaya au kifo.
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
Wakati wa Kuongeza Mafuta
• Zima injini na uwache injini ipoe kwa angalau dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko
cha mafuta.
• Jaza tangi la mafuta nje au katika eneo lenye hewa nyingi safi.
• Usijaze tangi la mafuta kupita kiasi. Ili uruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze hadi juu
ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
• Kagua tundu za mafuta, tangi, kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatayeyuka kabla ya kuwasha
injini.
Wakati wa Kuwasha Injini
• Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji hewa
(iwapo kipo) vimefungwa na kukazwa.
• Usiwashe injini wakati kiziba cheche kimeondolewa.
• Injini ikifurika, weka choki (ikiwa ipo) katika eneo la kuonyesha FUNGUA /
ENDESHA (OPEN / RUN), songeza kidhibiti injini (ikiwa kipo) hadi eneo la
kuonyesha HARAKA (FAST) na ushtue hadi injini iwake.
Wakati wa Kuendesha Kifaa
• Usiinamishe injini au kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
• Usijaribu kutoruhusu hewa kuingia kwenye kabureta ili kusimamisha injini.
• Usiwashe au kuendesha injini kamwe wakati uunganishaji wa kisafishaji hewa
(iwapo kipo) au chujio la hewa (iwapo lipo) vimeondolewa.
Wakati wa Kubadilisha Oili
• Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la mafuta
liwe tupu au mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
Wakati wa Kuinamisha Kifaa ili Kutekeleza Udumishaji
• Wakati unapotekeleza udumishaji unaohitaji kitengo kuinamishwa, tangi la mafuta,
iwapo limewekwa kwenye injini, lazima liwe tupu au mafuta yanaweza kuvuja na
kusababisha moto au mlipuko.
Wakati wa Kusafirisha Kifaa
• Safirisha tangi la mafuta likiwa TUPU au vali ya kufungia ikiwa katika eneo la
kuonyesha IMEFUNGWA (CLOSED).
Wakati wa Kuhifadhi Mafuta Au Kifaa Kilicho na Mafuta Kwenye Tangi
• Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vitu vingine ambavyo
vina taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto
kwenye mvuke wa mafuta.
Hatari ya kuvutwa nyuma kwa
haraka 
Hati ya kemikali 
Babuzi 
37

Advertisement

Table of Contents
loading

Table of Contents